Habari za Punde

Wilaya ya Chake Chake Yaongoza kwa Udhalilishaji.


Na Haji Nassor, Pemba

WILAYA Chake chake, imetajwa kuongoza kwa makosa ya udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto, ambapo katika kipindi cha kuanzia mwezi Juni 2011, hadi Machi mwaka huu, kuliripotiwa makosa 38 kati ya 51 yaliotokezea Mkoani humo.

Kwa mujbu wa taarifa hiyo, ilieleza kuwa wilaya Mkoani kulitokeza makosa 13 na kuizidi na wilaya ya Chake chake kwa makosa 25, ambayo hayo ni yale yalioripotiwa vituo vya Polisi vya Mkoani, Chake chake na Kengeja.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa wilaya ya Chake chake, kulitokeza makosa 11 ya ubakaji, na 11 ya kutorosha, vipigo kwa wanawake yalikuwa makosa tisa, waliopewa ujauzito yalikua makosa mawili, na wa kuingiliana kwa ndugu lilikua kosa moja.

Uchunguuzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi umegundua kuwa kati ya kesi hizo 11 za ubakaji, tano ziko Mahakamani na tano bado zinaendelea na upelelezi na moja ilifutwa kwa sababu mbali mbali ikiwa ni pamoja wahusika kumaliziana nje ya Polisi.

Aidha taarifa hiyo ikaeleza kuwa kati ya kesi hizo 11 za kutorosha, saba zinaendelea na upelelezi, wakati kesi moja imefungwa na kesi tatu ziko Mahakamani kwa hatua zaidi.
Kwa pande wa wilaya Mkoani kati ya makosa hayo 13 ya udhalilishaji wakijinsia kwa wanawake na watoto, kulikua na kesi nane za ubakaji, kutorosha, kulawiti, kumuigilia mlevu wa akili na kukashifu zilikua kesi moja moja.

Kati ya kesi hizo nane za ubakaji, tatu zinaedelea na upelelezi, mbili zimefungwa, tatu zimeshapandishwa Mahakamani na moja ya kutorosha inaendelea na upelelezi, wakati ile moja ya kumpa ujauzito mwanafunzi nayo imepandishwa mahakamani.

Kwa upande wake Katibu wa Mtandao wa Polisi wanawake Mkoa wa Kusini Pemba Sajent Zuwena Hamad Ali, alisema kwa upande wao kuanzia Januari 2012 hadi Febuari, walipokea kesi nne za ubakaji ambapo wilaya ya Mkoani na Chake chake zilikua na idadi sawa ya mbili mbli.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, Hassan Nassir alisema, Jeshi la Polisi kupitia Mtandao wake wa Polisi linaendelea kujipanga ili kutokomeza vitendo hivyo.

Alisema kupitia mtandao huo sasa watawanasa wanaopa ujazito wanafunzi na watu wengine, kwa vile wameanza kupeleka sampli ya damu kwa ajili ya vipimo vya vina saba (DNA) hospitali ya Muhimbili.

Kwa uapande wake Mkuu wa wilaya ya Chake chake, Mwanajuma Majid Abdallah alieleza kuwa suala la kudhibiti vitendo vya ukatili na udhalilishaji wa wanawake na watoto, linahitaji ushirikiano wa pande zote wakiwemo wazazi.

Nae Mratibu wa Mradi wa TUNAJALI kutoka Jumuia ya waliokatika mapambano dhidi ya Ukimwi Tanzania tawi la Pemba (Pemba) Ali Yussuf alisema kwa sasa wanakusudia kuanzisha mapango maalum wa kuwakinga watoto wakiwemo wanafunzi na vitendo mbali mbali vya udhalilishaji.

Suala la udhalilishaji wa wananawake na watoto bado limekua ni changamoto kubwa kutokana na jamii kuzioonyeshea vidole taasisi za Mahakama na Jeshi la Polisi wakidai kuwa hawajazipa kipuambele kesi za ain hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.