Habari za Punde

Maalim Seif atembelea wagonjwa

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiitikia dua wakati alipofika nyumbani kwa Mzee Ali Haji Pandu huko Mpendae kwa ajili yakumjuilia hali.) Picha na Salmin Said, OMKR

Na Hassan Hamad OMKR

Makamu wa Kwanza waRais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad leo alifanya ziara ya kutembelea wagonjwa na wafiwa mbali mbali katika manispaa ya mji wa Zanzibar.

Miongoni mwa wagonjwa aliowatembelea na kuwafariji ni pamoja na Mzee Ali Haji Pandu anayeishi eneo la Mpendae na Sheikh Habib Ali Kombo anayeishi Kiembesamaki.

Katika ziara hiyo , Makamu wa Kwanza wa Rais amewaombea wagonjwa hao wapone haraka ili waweze kujumuika katika shughuli za ujenzi wa Taifa.

Maalim Seif amekuwa na utaratibu wa kuwatembelea na kuwafariji wagonjwa na wafiwa mbali mbali Unguja na Pemba, katika jitihada zake za kuwa karibu zaidi na wananchi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.