Nyumba nambari
KS/MB/671A iliopo Mbweni inauzwa kwa mnada wa hadhara kwa idhini ya amri ya
Katibu Mtendaji,Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana, Zanzibar (Kumbukumbu
KWNMA/UR/T.166/1994/68).
Nyumba hiyo ni kubwa na
imekamilika. ina vyumba vitano (5) vyumba viwili ni self contained), kumbi
mbili, vyoo na varanda chini na juu kwenye kiroshani pamoja na uwanja wa uzio
(fence).
Nyumba ipo karibu na
pwani na Hoteli ya Mbweni ruins. Ipo jirani na nyumba za Bwana Ali Mayugwa, Mheshimiwa
Seif Sharif Hamad na Bwana Bushta.
Siku na tarehe ya mnada
itatangazwa na Kamisheni ya Wakfu baada ya siku kuu ya eid el fitri.
Kwa maelezo zaidi fika
katika Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana, Forodhani.
Ahsanteni
No comments:
Post a Comment