
Mgeni Rasmi katika Mchezo wa Kombe la Hisani kwa ligi kuu ya Grand Malt Zanzibar,Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii (SMZ),Mh. Juma Haji Duni (kushoto) akikabidhi Ngao hiyo kwa Nahodha wa Timu ya Jamhuri kutoka kisiwani Pemba,Ally Said Choma baada ya kuinyuka mabao timu ya Super Falcon mabao 3-1 katika mchezo uliopigwa jana usiku kwenye uwanja wa Amani,Zanzibar. Katikati ni Meneja Masoko wa Grand Malt, Fimbo Butallah

Na Salum Vuai, Maelezo
TIMU ya soka ya Jamhuri, imefanikiwa kubeba Ngao ya Hisani baada ya kuwakata kidomodomo mabingwa wa soka Zanzibar Super Falcon kwa kipigo cha mabao 3-1.
Katika mchezo huo wa uzinduzi wa ligi kuu ya Zanzibar msimu wa 2012/13 inayodhaminiwa na kinywaji cha Grand Malt, Super Falcon hawakuwa katika kiwango ca kuridhisha ambapo mlinda mlango wao Suleiman Janabi, alikuwa sababu ya moja kwa moja kwa mabao mawili kati ya hayo.
Pambano hilo lilifanyika katika uwanja wa Amaan wakati wa usiku na kupambwa na burudani mbalimbali za muziki, huku beni ya mbwa kachoka nayo ikirindima majukwaani.
Pamoja na kupoteza mchezo huo, Super Falcon ndiyo iliyokuwa ya kwanza kuzifumania nyavu za Jamhuri kwa bao la dakika ya 15 lililopachikwa kimiani na Deo Cassian, aliyeunganisha vyema mpira wa krosi kutoka kwa Hemed Bakari.
Jamhuri iliweza kusawazisha katika dakika ya 21 kupitia kwa mchezaji wake Mfaume Shaaban aliyeruka kupiga kichwa akiunganisha krosi ya juu iliyochongwa na Bakari Khamis.
Mabao mengine ya Jamhuri yalifungwa na Mbarouk Chande na Azori Ndege katika dakika za 25 na 83 mtawalia, yote yakitokana na uzembe wa mlinda mlango Janabi, ambaye baadae alipumzishwa na nafasi yake kuchukuliwa na Bakari Khamis.
Pambano hilo lilitanguliwa na mchezo wa burudani uliozikutanisha timu za FC Real ambayo ni bingwa wa Wilaya ya Mjini ngazi ya Junior, na kombaini ya wilaya hiyo ya wachezaji walio chini ya miaka 15, ambazo zilishindwa kufungana.
Mapema, kabla ya kuzindua pambano hilo kwa kupiga mkwaju wa penelti mbele ya Meneja Masoko wa Grand Malt Fimbo Butala, Waziri wa Afya Juma Duni Haji aliyemuwakilisha Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi, alizitaka timu za ligi kuu kuutumia vyema udhamini uliopatikana, kuonesha soka la kisasa na sio la kubutuabutua.
Alisema mchezo mzuri ni muhimu ili kuwafanya mashabiki waliopoteza mapenzi kwa soka la nchi yao, kuacha kizishabikia timu za Ulaya na badala yake warejeshe mahaba kwa timu zao
ikiwa kinywaji laini ( soft) kama koka cola kina pombe angalia http://www.metro.co.uk/news/903472-coca-cola-and-pepsi-contain-traces-of-alcohol,
ReplyDeletejee hii grand malt itakuwa haina kitu si kudanganyana tu ? na wewe waziri mzima wa afya unaenda kujumuika kwenye upotofu kama huu jee ni mjinga kuwa hujui? au mpumbavu hukutaka kufahamu? au mnataka wote tuwe walevi kama amani karume ? wenzenu ulaya wameamka wanajaribu kupiga vita ulevi, nyinyi ndio mnashabikia sasa