Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akikabidhi sare kwa Wanachama wa Vikudi vya Utamaduni vya Imarisha, Kibati na Big Star mara baada ya kuufungua Mkutano wa UVCCM Mikoa ya Magharibi na Mjini hapo ukumbi wa CCM Amani Mjini Zanzibar.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Tifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akiudungua Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Umoja wa Vijana wa CCM { UVCCM } wa Mikoa Miwili ya Magharibi na Mjini Hapo CCM Amani Mjini Zanzibar. Kushoto yake ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mjini Magharibi Ndugu Yussuf Mohd Yussuf.
Na Othman Khamis Ame OMPR
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi alisema Jumuiya za Chama Hicho zinaweza kukosa ufanisi kutokana na tabia ya baadhi ya Viongozi kudharau Wanachama waliokubali kujitolea kuimarisha Chama hicho.
Kauli hiyo aliitoa wakati akiufunguwa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM {UVCCM } wa Mikoa Miwili ya Magharibi na Mjini hapo katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya CCM Mkoa Uliopo Amani Mjini Zanzibar.
Balozi Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema ipo tabia chafu iliyojengeka ndani ya chama ya baadhi ya Wanachama kumuepuka mwanachama anayepoteza muda na nguvu zake kwa ajili ya kutetea na kukisimamia chama katika utekelezaji wa Sera zake.
Aliwataka Wanachama na Viongozi hao wa Umoja wa Vijana wa CCM {UVCCM} Kuhakikisha kwamba wanawachagua Wanachama wanaoelewa wajibu na dhamana zao katika Jumuiya na Chama chenyewe.
Alifahamisha kwamba Umoja huo wa Vijana pamoja na ule ya Wanawake { UWT } ndio mkono mkubwa na mrefu ndani ya chama cha Mapinduzi kwa sababu ya nguvu na wingi wao. Hivyo upo wajibu kwao kuhakikisha wingi na nguvu hizo zinalindwa na kuenziwa ipasavyo.
Aliwatahadharisha Vijana hao kuwa makini katika ulinzi wa Chama chao kwa vile zipo dalili zilizoanza kujichomoza za kuvamiwa kwa Jumuiya hiyo kwa malengo ya watu wachache wanaoelekeza nguvu zao katika uchaguzi wa urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wa Mwaka 2015.
“ Kinacholeta tabu hivi sasa ambacho Vijana wameanza kutumiwa ni nafasi ya Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Mwaka 2015.Msikubali Jumuiya yenu ikatumiwa kwa maslahi binafsi”. Alitahadharisha Balozi Seif.
Balozi Seif Aliwataka wanachama wote wenye nia ya kutaka kugombea nafasi hiyo ni vyema wakasubiri wakati utakapowadia na liliopo sasa ni kuendelea kushirikiana na viongozi wenye dhamana hiyo katika kuwaletea maaendeleo Wananchi.
Akigusia suala la Muungano Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif aliwakumbusha Vijana hao kwamba CCM Bado inaendelea kutetea sera za Serikali Mbili ambazo kila mpenda Maendeleo ameshahudia ufanisi uliopatikana.
Alisema wapo baadhi ya watu wanaochukia mfumo huo lakini alisisitiza kwamba wataendelea kuchukia kwa sababu mfumo huo bado unaonekana kupendwa na Wananchi pamoja na wanachama ambao ndio waamuzi wakati wa mchakato wa mabadiliko ya Katiba ya Muungano wa Tanzania.
Akimkaribisha Balozi Seif Ali Iddi Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM wa uliokuwa Mkoa Mjini Magharibi anayemaliza muda wake mh. Tauhida Galos Nyimbo aliwaasa Vijana kuelewa kwamba kazi ya Vijana ni ya kujitolea wakati wote.
Mh. Tauhida alisema kwamba tabia ya baadhi ya Wanachama kujaziwa fomu za Uongozi inadhoofisha nguvu za Chama kwa vile muda mwingi wa watu hao hutegemea kupata kipato zaidi badala ya kujitolea.
“ Tunaelewa waliojaziwa fomu wana hulka ya kuuliza posho la kikao kiasi gani, ajira lini pamoja na mshiko upo?”. Alifafanua Mh. Tauhida.
Mapema akisoma Taarifa fupi Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM wa uliokuwa Mkoa Mjini Magharibi Magharibi Ndugu Mohd Ali Khalfan alisema suala la uchumi bado linaoneka kuwa na matatizo ndani ya Jumuiya hiyo.
Hata hivyo Ndugu Mohd alisema kwamba Uongozi wa Jumuiya hiyo imejipanga vyema katika kukabiliana na tatizo hilo kwa lengo la kujitegemea wenyewe bila ya kusubiri mwega wa Chama chenyewe.
Akizungumzia amani Ndugu Mohd alifahamisha kwamba wapo watu baadhi ya watu na vikundi vinavyoendeleza tabia ya kupotosha Wananchi hasa katika amani na utulivu wa Nchi. Hivyo Jumuiya yao imeahidi kupambana na vitendo hivyo kwa kutangaza sera sahihi za chama cha Mapinduzi.
Katika Mkutano huo Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM alikabidhi zawadi za safe za chama kwa Vikundi vya Utamaduni vya Imarisha, Kibati pamoja na Big Star vilivyotolewa na Mwenyekiti huyo wa UVCCM wa uliokuwa Mkoa Mjini Magharibi kama ishara ya kumbu kumbu na upendo kwa wana CCM hao.
Huyu mzee mie simfahamu, yeye ndio anaetakiwa atatue kero za muungano mwaka wa pili huu kuna kero hata moja aliyoitatua?, jawabu hakuna anaona uongozi na kudanganya watu ili yeye apate kuvimbisha tumbo ni bora zaidi, kasahau kama kuna kufa na kutetea maslahi yake kwa kuwa anapata pesa za muungano kama mbunge, hajui kama ni mambo ya kupita tu, atwambie yeye ni makamo wa rais wa Zanzibar akitoka nje ya nchi anajulikana?, Rais wa Zanzibar akitoka akienda hapo kenya basi hajulikani?, atamwambie wafanyakazi katika wizara au ofisi au za Muungano wapo wazanzibar wangapi. wallahi hana jibu ya yote haya, anaona sawa tu kuwapa watu jezi za mpira watu wa maskani na kuwalemaza kiakili, bila ya kuwepo maendeleo yoyote anayotulea....VIONGOZI KAMA HAWA NDIO MAADUI WA MAENDELEO YA NCHI YETU....mie sipingi muungano napinga mfumo mzima wa Muungano uliopo, kwa maisha ya sasa hivi tunahitaji marekebishoi makubwa ya Muungano tushachoka na bla bla za kero za Muungano zinazoendelea kwa miaka 48 bila ya kutatuka na viongozi wanaotetea matumbo yao. mfumo huu wa Muungano ni baadhi ya viongozi tu ndio unaowafaidisha, utakuta kiongozi Mbunge, Waziri wa Munngano, Muwakilishi wa baraza la wawakilishi na kadhalika, tunataka utendaji hatutaki na tushachoka na bla bla zenu viongozi mabutu.....ndugu zangu wa CCM fikirieni na tuweni makini kwa mambo haya wasitudanganye hawa watu kwa kujifaidisha wao na family zao sisi tukafa na njaa.
ReplyDelete