Habari za Punde

Kizimbani kwa kuzidisha abiria


Na Madina Issa
JUMA Salum Karavani (28) mkaazi wa Mombasa Wilaya ya Magharibi Unguja pamoja na Shaibu Haroub Alawi (25) wamepandishwa katika kizimba cha mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe kwa kosa la kuzidisha abiria.

Ilidaiwa mahakamani hapo na mwendesha mashitaka wa serikali Said Mohamed mbele ya hakimu Sabra Mohamed kuwa mnamo Septemba 19 mwaka huu huko Mombasa Wilaya ya Magharib Unguja wakiwa dereva na utingo wa gari namba 825 ruti 512 wakitokea upande wa Mombasa  kuelekea Kisauni walipatikana wakiwa wamechukua abiria 23 badala ya 20 kwa mujibu wa uwezo wa gari lao,  hivyo kusababisha abiria watatu kuzidi kitendo ambacho ni kosa kisheria.

Kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 120 (1) (2) sheria namba  7 ya mwaka 2003 sheria ya Zanzibar.

Washitakiwa hao walikubadi kosa hilo na kuiomba mahakama iwapunguzie adhabu .


Mwendesha mashitaka Said aliiambia mahakama hiyo kuwa hawana kumbukumbu yoyote kwa washtakiwa kuhusika katika mashtaka mengine.


Hakimu Sabra aliwataka wa watoe faini ya shilingi 25,000 au watumikie kifungo cha wiki mbili na kuwambia hati ya rufaa ipo wazi kwa aliyekuwa hajaridhika na hukumu hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.