Habari za Punde

Mchuano mkali CCM leo


Na Mwantanga Ame
MCHUANO  mkali unatarajiwa kujitokeza leo katika uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kwenye ngazi ya Wilaya  ambao utategua kitendawili cha nani atabakia kuwa kiongozi ndani ya chama hicho.

Hali hiyo inatarajiwa kujitokeza baada ya wanachama wa CCM ngazi ya Wilaya kuwapigia kura wanachama wenzao waliojitokeza kuwania nafasi mbali mbali.

Wanachama hao wamo vigogo ambao wanatarajiwa kuonesha upinzani mkali baada ya kujitokeza sura mpya zinazotaka kuwania nafasi hizo ambapo uchaguzi huo utafanyika kwa wilaya zote.

Upande wa mkoa wa mjini uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika katika Wilaya mbili ikiwemo ya Mfenesini na Dimani.

Alizungumza na Zanzibar Leo, Katibu Mwenezi wa CCM, Mkoa wa Mjini, Maulid  Issa alisema uchaguzi huo utahusu nafasi za wanaowania Wenyeviti wa Wilaya, Wajumbe wa tano CCM Wilaya, Wajumbe sita wa Halmashauri Kuu ya Taifa Wilaya, Wajumbe watano wa Mkutano Mkuu wa Wilaya.


Wengine aliwataja kuwa ni Wajumbe wa nafasi za Katibu wa Wilaya, Mshika fedha na Uchumi ambapo mkutano wa Wilaya ya Dimani unatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mbweni na Wilaya ya Mfenesini utafanyika Beitrasi.

Baadhi ya majina yaliopitishwa kwa Wilaya ya Mfenesini ni Abdulaziz  Salum Abdulaziz, Abdi Mohammed Khamis, Ali Abdulla Ali, Alex Saimon Mwavangila, Jaffar Khamis Burhan, Babu Chiriku Pazi, Fatma Othman Ali, Huda Ali Karisa na Isaac Abraham Sepetu.

Wengine ni Chum Shuari Machano, Keis Mashaka Ngusa, Machano Othman Said, Machano Hassan Ali, Makame Khamis Kombo, Mbarak Soud Msabaha, Mohammed Abdaalla Khamis, Shawana Bukheit Hassan na Ussi Ame Randu.

Wagombea nafasi ya Mwenyekiti CCM Wilaya ya Dimani ni  Abdalla Faki Shunda (45), Amour Haji Nassor (63), Hussein Ali Kimti ( 52), huku wengine kwa ngazi ya Wilaya Ahmada Yahya Abdulwakil (54), Ali Hassan Khamis (69), Ali Suleiman Ali (SHIHATA) (57), Dogo Idi Mabrouk (41), Hussein Ali Khamis (46), Halima Tawakal Khairalla (55), Issa Saadalla Boi (69), Khamis Yahya Machano (52), Madai Hamad Makungu (52), Mohamed Hija Mohammed (62)
na Mwaka A. Ramadhan (52).

Wengine ni Matogo Juma Matogo (44),Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini (60),Shaibu Maalim Yussuf (49), Sira Ubwa Mamboya (57), Thuwaybah E. Kisasi (52), Zaina Ali Suleiman (47), Mwashamba Ali Juma (58), mkoa wa Mjini Unguja waliopitishwa kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Mkoa ni Borafia Silima Juma ( 70), Mussa Hassan Mussa ( 53)
Hassan Omar Mzee (64).

Wagombea Nafasi ya Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa  ni Maulid Issa Khamis ( 52), Nuru Mohamed Ahmeid ( 39), Sufiani Khamis Ramadhan ( 42) na
Wagombea nafasi ya Katibu wa Uchumi na Fedha Mkoa, Ahsante Haji Abdalla (38), Ramadhan Iddi Khamis (55)  na Mahmoud Thabit Kombo (42).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.