Habari za Punde

Nasaha kutoka kwa Muisamu


Leo ni siku ya Ijumaa ni siku adhimu kwa waislamu ambapo katika misikiti hukusanyika kwa ajili ya Sala na kuzungumzia masuala ya dini yetu.

Imesadifu Ijumaa hii kuwa ipo mfunguo tatu moja katika miezi muhimu na mitakatifu katika Uislamu. Wakati Mahujjaaj wako katika miji mtakatifu ya Makkah na Madina wakitekeleza Ibada hii adhimu – nguzo ya tano katika Uislamu.

Tunapenda kuwanasihi Waislamu na waumini kwa ujumla kuipitisha siku hii kwa salama na amani na kwa utulivu na masikitiko yetu yote tumshtakie Allaah Suhaanahu Wata’ala ambae ni mbora wa kuhukumu. Tusijiingize katika vitendo vyovyote vitakavyoharibu jina la Dini yetu, utukufu wa Mola wetu na ubora wa Mtume wetu rehma na amani ziwe juu yake.

Tukumbuke kila tutakalolifanya hapa duniani Allaah Subhaanahu Wata’ala anatuona na atakwenda kutuuliza siku ya masiku.

Ndugu yangu katika Imani, Muislamu mwenzangu nnakuusia kama nnavyoiusia nafsi yangu kumuogopa na kumcha Allaah Subhaanahu Wata’ala hivyo usishiriki wala kujihusisha na tukio lolote uvunjifu wa amani katika siku hii ya leo. Nenda kafanye Ibada kisha endelea na shughuli zako huku ukimuomba Allaah Subhaanahu Wata'ala aturudushie amani na utulivu katika visiwa vyetu.

1 comment:

  1. hakika umesema kweli kwa sababu watu wanasahau kama Mlipaji hafi na wala mkaguzi wa Amali za waja hasinzii anaona kila kiti na kila kitu kitakwenda kuhesabiwa na kulipwa tusihadaike na uluwa pamoja na pumzi. hivyo vyote ni neema na tunapaswa tutumie neema za Allah vile inavyotakiwa

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.