Kaimu Mkurugenzi wa Islamic Benki Mohammed Khalfan Zahor, ( kulia) akimkabidhi msaada wa saruji tani 4 Mwalim Mkuu wa Madrasatul Munawar Islamiyya Malindi Ust. Abeid Mahfoudh Khamis (kushoto) na Sheha wa Malindi akishuhidia,makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja vya madrasa hiyo Malindi mjini Zanzibar leo.
Kaimu Mkurugenzi wa Islamic Benki Mohammed Halfan Zahor, akitowa maelezo ya Islamic Benki katika hafla ya kukabidhi saruji kwa ajili ya Madrasatul Munawar Islamiyya Malindi Zanzibar, Islamic Benki hutowa misaada kwa jamii.
Mwalim Mkuu wa Madrasatul Munawar Islamiyya Malindi Ust. Abeid Mahfuodh Khamis, akitowa shukrani kwa Uongozi wa Islamic Benki kwa kutoa msaada huu kwa wakati muafaka na kujali jamii kwa kutowa misaada ya hali na mali kuendelea madrasa hiyo katika kumalizia ujenzi wake ili kutowa nafasi kwa wanafunzi wao.
Mwalimu Mkuu Msaidisi wa Madarasatul Munawar Islamiyya Malindi Ust. Tahir Muhidin, akitowa historia ya madrasa hiyo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Islamic Benki, wakati wa kukabidhi msaada wa saruji kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa madrasa hiyo kutowa nafasi kwa Wanafunzi.
Mbona Naibu Mkurugenzi wa Benki hakuvaa viatu.
ReplyDeleteMie mjukuu wa sheha .Mie huyo sheha babu yangu mzalia mama niemekaa miaka miwiwli kwake ( zanzibar) pia nimesoma madrasatul munawwar ust.abeid ndio ustadh wangu pia ustadh tahir ...
ReplyDelete