Habari za Punde

Kiongozi wa Timu ya Jangombe Boys Ali Othman Kibichwa adai kupigwa na Kiongozi wa ZFA Wilaya .

 Hapa ndipo nilipopigwa ndivyo inavyoonekana akisema huku akiwaonesha waandishi  alipofika uwanja wa Amaan kuangalia mpira wa ligi kuu ya Zanzibar.  
 Kiongozi wa timu ya Jangombe Boys Ali Othman Kibichwa akizungumza na waandishi wa habari za michezo Zanzibar kutokana na kitendo cha kupigwa na Mjumbe wa ZFA Wilaya ya Mjini Uledi Said, akipinga kitendo hicho cha kushambulia wakati akidai siku ya mchezo wake na timu ya Kilimani City  ulichezeshwa kwa upendeleo.
 Kiongozi wa Timu ya Jangombe Boys Ali Kibichwa akitowa malalamoko yake kwa Kiongozi wa ZFA Wilaya ya Mjini Hassan Chura kutokana na kitendo cha mjumbe wa ZFA Uledi kuchukua hatua ya kumpiga kama anavyodai kiongozi huyo.wakiwa katika uwanja wa Amaan.
Mwenyekkiti wa ZFA Wilaya ya Mjini Hassan Chura akisoma barua ya Polisi inayoamuru kuitwa Kituoni Kiongozi wa ZFA Wilaya ya Mjini Uled  Said, wakati alipofika Ofisi za ZFA Wilaya ya Mjini kulalamikia kuonewa wakati wa mchezo wao na timu ya Kilimani City , timu hizo zimetoka sare ya bila ya kufungana.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.