Habari za Punde

Wawi Star yatinga 8-bora

 
Na Abdi Suleiman, Pemba
 
TIMU ya Wawi Star ya Chake Chake, imefanikiwa kuungana na ndugu zao wa Mkungu Malofa, kucheza hatua ya nane bora, kwenye ligi daraja la pili taifa.
 
  Wawi Star ilimudu kuitandika Kichungwani City magoli 2-0, katika mechi ya ligi hiyo Wilaya ya Chake Chake, hatua ya sita bora, ikifungiwa mabao yake na Nassor Iddi pamoja na Abdallah Othman, mnamo dakika za 85 na 89.
 
Hata hivyo, kipigo hicho kiliwakasirisha sana mashabiki wa Kichungwani, walioanza kuwatupia shutuma viongozi wao kwa madai kuwa wameihujumu timu hiyo, kwa kuuza mchezo huo.
 
Baadhi ya wachezaji walisikika wakidai kuwa hawatajisajili tena katika timu hiyo msimu ujao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.