Habari za Punde

Ziara ya Dk Shein Mkoa wa Kusini Pemba

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata malezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji ZAWA,Dk.Mustafa Ali Garu,alipotembelea shughuli za ujenzi wa Tangi la Maji safi,katika mradi wa maji vijijini uliofadhiliwa na Benki ya maendeleo ya Afrika,(ADB)huko Gombani,akiwa katika ziara ya Mkoa wa KusiniI Pemba jana
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji ZAWA,Dk.Mustafa Ali Garu,(kushoto)akitoa maelezo ya michoro ya kazi ujenzi wa Tangi la Maji safi,katika mradi wa maji vijijini uliofadhiliwa na Benki ya
maendeleo ya Afrika (ADB)kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) alipotembelea shughuli hizo jana huko Gombani,akiwa katika ziara ya Mkoa wa KusiniI Pemba jana
 Mkurugenzi Mkuu shirika la Utangazaji ZBC Hassan Abdalla Mitawi,akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) alipotembelea shughuli za Digital katika kituo cha Tv Mkanjuni Pemba, akiwa katika ziara ya Mkoa wa Kusini Pemba jana
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Agape Association Ltd, Dr.Vernon Fernanders,akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na ujumbe wake kuhusu kutoka Analogi kwenda Dijital katika kituo cha Tv Mkanjuni Pemba jana,wakati wa Ziara
ya Rais kuangalia shuhuli mbali mbali za maendeleo katika Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Agape Association Ltd, Dr.Vernon Fernanders,akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,namna ya king'amuzi kinavyoweza kufanya kazi wakati wa kuanza kutumia Digital alipotembelea kituo cha
Tv Mkanjuni Pemba jana,wakati wa Ziara ya Rais kuangalia shughuli mbali mbali za maendeleo katika Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba Hamadi Bakari Mshindo,alipowasili katika viwanja vya Ofisi ya Mkoa wa Kusini Pemba, akiwa na ujumbe wake kupata taarifa ya kazi za mendeleo ya Mkoa huo,alipoaanza ziara ya kuangalia miradi mbali mbali ya maendeleo
 Baadhi ya Viongozi walioungana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika ziara Mkoa wa Kusini Pemba,wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Meja Mstaafu Juma Kasim Tindwa,(hayupo pichani) alipokuwa akisoma Ripoti ya kazi za maendeleo ,wakati ais alipoanza Ziara hiyo ya kuangalia maendeleo ya miradi mbali mbali
 Baadhi ya Wananchi na Viongozi waliohudhuria katika Mkutano wa Utoaji wa taarifa ya Ripoti ya kazi za maendeleo, kwa Mkoa wa Kusini Pemba,wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Meja Mstaafu Juma Kasim Tindwa,(hayupo pichani) akisoma ripoti hiyo mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, alipoanza ziara hiyo ya kuangalia maendeleo ya miradi mbali mbali jana
 Mkuu wa Mkoa Meja Mstaafu Juma Kasim Tindwa,akisoma Ripoti ya kazi za maendeleo, kwa Mkoa wa Kusini Pemba, mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, alipoanza ziara hiyo kwa kupokea taarifa hiyo na kuweza kuangalia miradi mbali mbali ya maendeleo ndani ya shehia na wilaya za Mkoa wa Kusini Pemba jana
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, alipokuwa akizungumza na wakati wa kupokea taarifa ya ripoti ya kazi za maendeleo ndani ya Mkoa wa Kusini Pemba jana,iliyoanza kwa wilaya ya Chake chake
Mfanyakazi wa Shirika la Umeme Pemba Shaibu Hassan,alipokuwa akitoa malalamiko yake mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, kuhusu ubadhirifu Fedha ndani ya Shirika hilo,wakati wa utoaji wa Ripoti ya kazi za Mkoa wa Kusini
Pemba,wakati wa Ziara ya kuangalia maendeleo ya miradi mbali mbali,ambayo ikiwemo iliyoanzishwa na wananchi.

[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

1 comment:

  1. Safari hizi ni moja ya ubadhirifu wa mali za umma. Hebu tuangalie safari ya rais na mawaziri karibu ya wote wako Pemba na kila mmoja kati yao anafurahia posho wala hakuna jipya. Jee tutafika?

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.