Habari za Punde

Ali Akiieleza kwa Waandishi ubunifu wake.

KIJANA Ali Mahmoud, mkaazi wa Tomondo Zanzibar, akitowa maelezo ya mashine ambayo ameibuni kwa ajili ya kuzalisha umeme wa upepo. Alifika katika ofisi  za Gazeti la Zanzibar Leo  kuonesha Utaalamu wake na kuomba msaada wa kuweza kufanikisha ubunifu wake huo ambao unahitaji shilingi millioni 40, ili kufanikisha ubunifu huo.

Ali amesema tayari ameshakwenda kwa Waziri Mbarawa Dar-es- Salaam, kuomba kupatiwa msaada kwa wataalam wa fani hiyo ili kufanikisha ubunifu wake na kuendeleza kipaji hicho na kuliletea Taifa sifa. 

Vijana kama hawa Serikali inahitaji kuchukua hatua za kuwasiadia na kuwaendeleza kielimu ili kupata vijana wenye ubunifu wa vitu mbalimbali.
 
Amesema anaendelea na ubunifu wake kwa kupata misaada kupitia kwa wahisani na kufika hatua hii ya ubunifu wake  
Amesema anahitaji msaada wa Serikali ili kufikia azma yake ya kumalizia mashine hii itakayoweza kuzalisha Umeme wa Kw 40.  

1 comment:

  1. haya msisema hatuna wabunifu au akili , chunguzeni mradi wa huyu kijana kama unaweza kuleta tija , mpatieni hizo fedha na utafiti zaidi ili tuondokane na umeme wa watanganyika. Serikali ilikuwa na fedha za kuchunguza kikombe cha babu , lakini hapa najua petu pakavu , chachandu mpopo....

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.