Na Salum Vuai, Dar es Salaam
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, leo aliwaongoza maelfu ya Watanzania katika sherehe za maadhimisho ya miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Sherehe hizo zilifanyika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi wote wa kitaifa nchini, mawaziri wa Serikali ya Muungano na ile ya Mapinduzi Zanzibar, viongozi wa ngazi zote na watendaji wakuu pamoja na wananchi mbalimbali.
Baadhi ya viongozi hao ni pamoja na Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Kwanza na wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad na Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, na Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Peter Pinda.
Wengine ni Marais wastaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi na Benjamin William Mkapa, Rais mstaafu wa Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume, Mawaziri Wakuu wastaafu Fredrick, Sumaye, Edward Lowasa na John Malecela, Spika wa Bunge Anne Makinda na Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho na viongozi wengine.
Pamoja na mvua ya wastani iliyokuwa ikinyesha mapema asubuhi, wananchi mbalimbali walijitokeza kwa wingi uwanjani hapo kusherehekea Muungano huo wa kihistoria ulioziunganisha nchi za Tanganyika na Zanzibar Aprili 26, mwaka 1964.
Shamrashamra mbalimbali zilipamba sherehe hizo, likiwemo gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama, halaiki ya muungano wa wanafunzi kutoka Zanzibar na Bara, ngoma za asili, Sindimba kutoka mkoani Lindi, Gonga-Kusini Pemba na Nyaketari kutoka Tarime, Mara.
Aidha, kikosi cha kwaya cha JKT Msange kutoka mkoa wa Tabora, nacho kilishuka uwanjani kuhitimisha maadhimisho hayo, ambapo kilitia fora kutokana na manjonjo ya kiongozi wake aliyekuwa kivutio kikubwa uwanjani hapo.
Mapema baada ya kuwasili uwanjani hapo, Rais Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi wa maadhimisho hayo, alipigiwa mizinga 21 na kukagua vikosi vya gwaride, kabla kupokea saluti ya utii kwa Rais.
Baada ya hapo, vikosi mbalimbali vya gwaride vilipita mbele ya mgeni rasmi na waalikwa wengine, kwa mwendo wa polepole na ule wa haraka, huku vikishangiriwa kwa nguvu na wananchi waliovutiwa na ukakamavu wa wapiganaji hao.
Kwa upande wao, vijana wa halaiki walinogesha sherehe hizo kwa kuonesha sura nne za maonesho, ambayo ni ulinzi, uchumi, afya na utamaduni, na kumalizia kwa sarakasi iliyowafurahisha wageni na wananchi wote waliohudhuria sherehe hizo.
Miongoni mwa maumbo waliyotengeneza na kufurahisha umma, ni maandishi yaliyosomeka “Miaka 49 ya Muungano”, pamoja na “Tusichanganye Kiswahili na Lugha nyengine”.
Tukio jengine lililosisimua hadhira uwanjani hapo, ni maonesho ya ndege za kivita za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), zilizoruka katika anga ya uwanja huo, huku zikitoa moshi wenye ishara ya bendera ya Taifa.
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliasisiwa Aprili 26, 1964 kutokana na makubaliano ya Rais wa kwanza wa Tanganyika Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyeyere, na aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Abeid Amani Karume.
Sherehe za mwaka huu zinabebwa na kaulimbiu isemayo, “Amani, utulivu na maendeleo ni matokeo ya muungano wetu, tuulinde na kuutunza.
IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
Ni siku kama siku nyengine tu za kawaida ila zaidi watanzania wanaendelea kuburuzwa katika muungano uliojaa usiri na ukiukwaji wa sheria.
ReplyDeleteMasuala mengi ya muungano ukiuliza badala ya kujibiwa unaambiwa wewe unataka kuuvunja. Hakuna kiongozi anaeweza kutoka hadharani akazungumza faida za muungano ambazo zitawakinaisha watu kwamba kweli hizi ni faida ambazo hazipatikani katika nchi nyengine ambazo hatuna muungano nazo.
Nyingi ya faida utakazotajiwa ni vitunguu, kuoana, mbatata, udugu wa damu.... vitu ambavyo hata watanzania wanaoishi nchi za nje kama vile usa, canada, australia, uk, n kwengineko ambako sheria na haki za binadamu zinaheshimiwa ni vitu vya kawaida tu na ni lazima kila raia apewe.
Tunaomba ALLAH atupe kila lenye kheri nasisi ili tuweze kumuabudu yeye.
Hivi siku kuu kama hizi zinazoangukia siku ya Ijumaa inakuwaje kwa Waislamu wanaotaka kwenda kusali Ijumaa na huku wanatakiwa wawepo kwenye gwaride au uwanjani?
ReplyDeleteAu Sala inakuwa si muhimu kwa siku hii? Sala hii ni Fardhu Ayn - Fardhu ya lazima kwa kila Muislamu au sivyo?
Mtasema sana!
ReplyDeleteMuungano upo na utaendelea kuwepo kwa uwezo wa M/Mungu!
Pamoja na mambo mengine, muungano ni matokeo ya 'ukhanithi'waliokuwa wakitufanyia Babu zenu'waarabu' kabla ya mapinduzi..tusingefikia kwenye muungano huu!
Leo hii mnajifanya mna dini sana..eeh? wakati ule waarabu wanatuadhibia wazee wetu mlikua kimyaaa! na masheikh na maulamaa walikua wamejaa kila pembe ya Z'bar...tutakwenda hivi..hivi!
"Asiyeutaka..ahame"
@Mtasema Sana
ReplyDeleteUna ushahidi wa unaoyaongea sisi tunajuwa from Day one muungano haukuridhiwa na Wazaznibari na ndio maana mzee karume akawa na upinzani kwa nyerere na mpaka sasa wanaong'ang'ania muungano ni watanganyika mimi nna uhakika wewe ni mmoja wao, na kasumba za kuwa waarabu waliwafanya watu watumwa, kwa taarifa yako hizo ni propaganda ambazo mpaka leo hakuna mzanzibari ambaye anaweza kujitokeza kutueleza kuwa yeye au mzee wake alifanywa mtumwa. Wazee wenu ndio walikuwa wakiwakamata na kukuuzeni na waarabu walikuwa wafanyabiashara na wanunuzi walikuwa wazungu ambao ndio waliowatumeni
kwa kuongezea ushahidi wa kuwa hao watumwa waliuzwa kwa wazungu ni umati mkubwa wa watu wenye asili za kiafrika katika nchi za caribbean, amerika kusini na kaskazini. Anyway huu muungano ambao hautakiwi ya nini kupoteza mabilioni ya pesa kusheherekea? wakati kwanza hautakiwi , la pili kuna mambo mengi yangefanyika kwa hizo fedha za sherehe kama kununua madawa hospitali, kukarabati mashule , kulipa madeni ya walimu na wafanyakazi wengine wa serikali , kutengeneza mabarabara mabovu katika miji yote
ReplyDelete