Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi akizindua rasmi mashindano ya Zaweda Cup yanayofanyika katika Jimbo la Kitope na kushirikisha pia Timu rafiki zilizo nje ya Jimbo hilo.
Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seiof akionyesha umahiri wake wa kupiga Penalti wakati akizindua rasmi mashindano ya ZAWEDA Cup hapo uwanja wa michezo wa Kitope.
Balozi Seif akitoa zawadi na baadhi ya vifaa kwa wawakilishi wa Timu za soka zinazoshiriki mashindano hayo ya ZAWEDA Cup yanayoendelea ndani ya Jimbo la Kitope.
Vijana wa Timu ya Soka ya New Stars ya Kiwengwa wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kupambana na Kibweni Yourth Organization kwenye pambano la uzinduzi wa mashindano ya Zaweda Cup Jimboni Kitope.
Timu machachari ya Kibweni Yourth Organization inayoshiriki mashindano ya Zaweda Cup wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kupambana na mabingwa watetezi wa Mashindano hayo New Stars ya Kiwengwa.Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Othman Khamis AmeOfisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Wanamichezo Nchini wametakiwa kuzingatia kanuni ya taratibu za michezo ili ziwawezesha kutekeleza vyema zile sheria 16 za mchezo wa soka sambamba na kujenga mfungamano wa upendo na urafiki miongoni mwao na hatiame kuenea ndani ya Jamii yote kwa ujumla.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akiyafungua mashindano ya mchezo wa soka ya ZAWEDA Cup yaliyoshirikisha timu 12 za jimbo la kitope pamoja na timu rafiki ambayo yameandaliwa na Jumuiya isiyo ya Kiserikali ya ZAWEDA.
Balozi Seif alisema Viongozi pamoja na Taasisi tofauti huamua kuanzisha mashindano mbali mbali kwenye maeneo tofauti ili kuwaunganisha pamoja wana michezo pamoja na kuibua vipaji vya Vijana.Alisema kinachohitajika zaidi katika Nyanja za michezo ni kudumishwa kwa uanamichezo ambao huleta upendo pamoja na uhusiano mzuri baina ya vikundi, watu na hata mataifa mbali mbali.
Balozi Seif ambae pia ni Mbunge wa Jimbo hilo la Kitope aliwataka wanamichezo hao kudumisha nidhamu katika mashindano hayo ili kulijengea sifa bora jimbo hilo katika Nyanja za michezo.Katika kuwahamasisha wana michezo hao Balozi Seif aliahidi kutoa Seti ya TV na king’amuzi chake, Jezi, Kikombe ,mipira pamoja na fedha Taslim shilingi laki 300,000/- kwa Timu ya soka itakayoibuka kuwa mshindi wa kwanza katika mashindano hayo.
Halikadhalika Balozi Seif akiwahamasisha wana michezo hao pia aliahidi kuwa mshindi wa Pili atazawadiwa Jezi, Mipira na Shilingi laki 150,000/- , mshindi wa Tatu Jezi, mpira mmoja na shilingi 75,000/-.“ Nitahakikisha kwamba Timu zote shiriki nitazipatia mpira mmoja.
Hiyo itakwenda sambamba na zawadi kwa Mchezaji, Bora, Mfungaji bora na mchezaji mdogo kuliko wote katika mashindano hayo “. Alisisitiza Balozi Seif.Mapema Mwakilishi wa Jimbo la Kitope Makame Mshimba Mbarouk aliwatahadharisha wanamichezo hao kuacha tabia ya kuufanya uwanja wa michezo kuwa sehemu ya masumbwi.
Mshimba alisema tabia za baadhi ya wachezaji kuchukuwa sheria mikononi mwao wakati muamuzi wa mchezo anakuwepo kiwanjani haistahiki kuendelea na inafaa kupiga vita mara moja kwa vile inaondosha heshima ya michezo.“ Taratibu za kuendesha michezo na hasa ule mchezo wa soka zimo ndani ya sheria 16 za mchezo huo kimataifa ambazo zinamuajibisha mwanamichezo yeyote aliyejikubalisha kuwemo ndani ya chungu hicho analazimika kuzifuata vilivyo “.
Alisisitiza Makame Mshimba.Katika Taarifa yao washiriki wa mashindano hayo iliyosomwa na Katibu wa Kamati tendaji wa ZAWEDA Cup Rashid Talib alisema lengo la kuanzisha mashindano hayo yaliyoasisiwa tarehe 16 juni mwaka 2012 ni kuibua vipaji vya vijana katika sekta ya michezo.
Rashid alisema katika hatua hiyo Jumuiya hiyo inayosimamia mashindano hayo ya ZAWEDA imekusudia kujenga chuo cha mradi wa kuviendeleza vipaji vya vijana ambavyo hatimae vitawapatia fursa za ajira badala ya kutegemea Serikali Kuu.
Katibu wa Kamati tendaji wa ZAWEDA Cup Rashid Talib kwa niaba ya viongozi wenzake pamoja na wanamichezo hao wamempongeza Mbunge wa Jimbo la Kitope, Mwakilishi na Kampuni ya Bopar kwa uamuzi wao wa kudhamini mashindano hayo muhimu.
Katika uzinduzi huo wa ZAWEDA Cup Balozi Seif pia alitoa zawadi za vifaa kwa timu zote 12 zilizokubali kushiriki kwenye mashindano hayo yanayoingia katika awmu ya pili sasa.
Timu hizo shiriki kutoka Jimbo la Kitope zikikaribisha pia Timu rafiki kutoka wilaya mbali mbali za Unguja ni Mabingwa watetezi wa mashindano hayo Timu ya Soka ya New Star ya Kiwengwa, Kibweni Yourth Organization ya Wilaya ya Magharibi na wenyeji Kitope United.Nyengine ni Mahonda Union, Mwache Alale, African Coast,
Fujoni Boys, Zaweda, Mahonda Kids, Mgambo Stars, Kilimani City ya Wilaya ya Mjini pamoja na Mbuyuni Stars.Katika uzinduzi huo Mbingwa watetezi News Stars ya Kiwengwa waliovalia jezi rangi nyekunda walipambana na Kibweni Yourth Organization katika pambano kali na la kusisimua lililokuwa gumzo kwa walioshuhudia na kuelezea faraja yao kutoka na mchuano huo mkali wa aina yake.
Matokeo ya pambano hilo lililomvutia mgeni rasmi Balozi Seif akishuhudia pamoja na waalikwa wengine lilimalizika dakika tisini zikiwaacha wababe hao wa New Stars ya Kiwengwa na Kibweni Yourth Organization wakitoa nguvu sawa kwa kufungana goli 2-2.
Othman Khamis AmeOfisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
serikali naona ina fedha kwa mambo ya kipuuzi, lakini haina pesa kwa mambo muhimu, chungeni wananchi hawa hawakutakieni heri wanataka kukutieni kwenye mambo ya michezo na anasa ili kukusahaulisheni kufatilia mambo muhimu ya kimaisha
ReplyDeleteMichezo kwa dunia ya sasa sianasa bali niajira na mtaji kwa vijana ndugu yangu tunge iomba serekali itilie mkazo, kufua,tim zetu na michezo mengine kama kuogelea ,na karati,gofu,na mengineo, kuliko, kungoja ujinga, wamuamsho. Michezo tulio izarau hapa Zbar ni utajiri kwa wenzetu
ReplyDeletenakusikitia mhadim , nakubaliana na mchangiaji number 1 , kama ungejua katika hao mamilioni ya wachezaji ni wangapi wamefanikiwa na huo utajiri unazungumzia? unasahau kuwa kuna elimu , afya , maji , umeme na mambo muhimu kimaisha unataka serikali iwekeze kwenye michezo? kwa wenzetu hayo niliyoyataja kwao washamaliza hata wakikaa kutwaaaa kucheza bao wao hawana hasara ndugu yangu wee ,
ReplyDeleteHili la afya na elim, tumeshindwa zamani, tangu serakali hata sisi wenyewe raia, wazanzibari hatuna utamaduni wa kupenda elimu, nipemfano mmoja,kijiji kipi au willaya wananch walokaa kutafakari suala la elimu ya watoto wao,nizogo na kugombea miskiti,Hata hawa, muamsho, hatujawasika hata siku moja, wanch tuchangie, afya na eliu, hawajui kazi hiyo, hufanywa nakila mzalendo aneye itakia mema jamii yake
ReplyDeletenafikiri unahitaji elimu ya uraia ndugu yangu, kazi ya serikali ni kukusanya kodi na mapato , na baadae kuyaelekeza yale mapato katika mambo muhimu ya kijamii , kwa hio suala la elimu , afya , maji , umeme na mahitaji yote muhimu ya kijamii ni wajibu wa serikali kutimiza. Wananchi wana hiari kuchangia ziada. Si suala la wananchi kutafakari , ni suala la serikali , wananchi kwanza wanashughulikia masuala ya chakula , maji na nk kutwa unafikiri watakuwa na muda huo , asubuhi tukiamka tunakimbilia kutafuta riziki na kubeba madumu kutafuta maji. Wananchi tunakatwa kodi a kutosha ,lakini viongozi wetu hutuibia kwa njia mbalimbali kujenga majumba nchini na nje , kupeleka watoto wao shule nzuri kwa mapato yetu. Wakienda kwenye vikao lazima wapate sitting allowance , jee hii ni lazima , hawa viongozi kukaa vikao ndio sehemu ya kazi zao sasa allowance ya nini? tafadhali kasome ndugu mhadim muda bado upo
ReplyDelete