Habari za Punde

JKU vinara netiboli Unguja

Na Mwajuma Juma
TIMU za netiboli za JKU wanawake na wanaume, zimeibuka vinara wa ligi ya mchezo huo Zanzibar kanda ya Unguja, iliyomalizika juzi.

Katika ligi hiyo iliyoshirikisha timu 12, saba za wanawake na nne za wanaume, JKU imetia mkobani pointi nane na dada zao walifikisha pointi 11 na zote kushika nafasi za kwanza.

Polisi wanaume imeibuka katika nafasi ya pili kwa kuwa na pointi sita na Mafunzo kwa wanawake, wakashika nafasi ya pili kwa kupata pointi 11 ikizidiwa kwa magoli.

Timu hizo zitakuwa kati ya timu nane za Unguja zitakazoungana na timu nyengine nane kutoka Pemba, kucheza ligi kuu ya Zanzibar.

Timu za wanawake ni JKU, Mafunzo, Valantia na Zimamoto, wakati kwa wanaume ni JKU, Polisi, Msambweni na Sogea.

Ligi kuu ya Zanzibar ya Netiboli inatarajiwa kufanyika kisiwani Pemba mwezi Agosti mwaka hu

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.