Habari za Punde

Maalim Seif : Wazanzibari kudai mamlaka ni haki yao

 
Hassan Hamad, OMKR
 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, ameunga mkono kauli iliyotolewa na Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano Zanzibar Eddi Riyami ya kuwataka Wazanzibari wasiotaka mamlaka kamili ya Zanzibar wajitokeze hadharani kama wanavyofanya wale wanaodai mamlaka kamili ya Zanzibar.
 
Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF ameeleza hayo katika viwanja vya Kibanda maiti mjini Zanzibar katika mkutano wa hadhara uliolenga kusherehekea “Umoja wa Wazanzibari”ulioasisiwa kufuatia maridhiano ya kisiasa.
 
Amesema hatua ya Wazanzibari kudai mamlaka ni haki yao, na kwamba hakuna dhambi ya kudai jambo hilo.
 
Amefahamisha kuwa wazanzibari walio wengi wameungana kudai mamlaka ya nchi yao kwa njia ya amani na demokrasia, na kutoa wito kwa wale wasiotaka mamlaka ya Zanzibar wajitokeze hadharani.
 
Amewahakikishia wananchi kuwa hatorudi nyuma katika kuitetea Zanzibar kuwa na mamlaka yake, ili iweze kutambulika kimataifa na kuweza kuratibu na kushughulikia mambo yake ya nje.

Kwa upande wake Katibu wa kamati ya maridhiano Ismail Jussa Ladhu, amewaomba viongozi wa vyama vyote kushirikiana na wananchi katika kudai mamlaka ya nchi, ili wazanzibari waweze kujikomboa kutokana na kile alichokiita ukoloni wa Tanganyika.
 
Katika risala ya wananchi wa mikoa mitano ya Zanzibar iliyosomwa na Ameir bin Ameir kutoka Bwejuu, amesema pamoja na mambo mengine, katiba mpya izingatie uwepo wa Jamhuri ya Zanzibar na uraia wake.
 
Mambo mengine waliyotaka yatolewe katika orodha ya mambo ya Muungano ni pamoja na sarafu, benki kuu, mambo ya nje, vyama vya siasa, baraza la mitihani pamoja na mafuta na gesi.

8 comments:

  1. Huyu mzee, kazi alizopewa hafanyi, kazi uchochezi tu!

    Tuone 2015 vurugu zikianza kama hatakimbilia hukohuko bara. Unguja panaaminika!

    ReplyDelete
  2. Please keep your mouth shut

    ReplyDelete
  3. Abaa, hicho kizungu si ungekitumia kufundisha nduguzo wa fom 6,..naona laa wafeli!

    Au nkizungungwa cha Bahamadi hicho cha kudia Nkataba?

    Baratu, pigani kelele ela nchi haitoki

    ReplyDelete
  4. Huyu Babu, kwa anavyoungwa mkono, angekua kweli ana nia ya kuisaidia Z'bar nadhani ingekua mbali sana.

    Lakini badala ya kuwahamasisha Wapemba matajiri pale DSM, wabunge na wawakilishi wake kusaidia maendeleo ya elimu, yeye anawaambia kua hiyo ni kazi ya serikali.

    Sijui atakuja kuongoza nchi ya aina gani( kama akipewa) ambayo watu wake hawana moyo wa kujitolea. watoto wanafeli kila leo kwa kukosa walimu wazuri wa sayansi.

    Hivi kweli mbunge anashindwa kuleta mwalimu wa hesabu au chemistry kutoka bara angalau mara 2 kwa mwezi kuja kupiga 'lecture'?

    Na hili inaonekana ni tatizo la W'bari wengi manake inashangaza kuona viongozi wengi wa SMZ wamesoma Lumumba lakini wameshindwa kuunda umoja wa wanafinzi wa zanmani wa lumumba kusaidia angalau vitabu.

    Viongozi kama Dr. Salim, Bilal, A.Karume, Maalim Seif wao wapo tu..visiwa vimelaaniwa vinataka duaaaa!!

    ReplyDelete
  5. Anonymus 9;40am , ni kweli kazi ya elimu ni ya serikali, huwezi kuwa unategemea fedha za matajiri ambazo wamezipata kwa shida nyingi kusaidia elimu , hilo ni jambo la hiari kama watataka kusaidia au laa, lakini serikali ni wajibu wake kuhakikisha elimu inayotolewa ni nzuri na inafundishwa na walimu wajuzi , ukitaka kujua ukweli elimu imekufa kutokana na sera za CCM ambao walikuwa wanpeana nafasi za ualimu na kuenda vyuoni kwa kuangalia siasa badala la uwezo wa wanafunzi wanaopelekwa chuoni.Ukirudi nyuma angalia vyuo na shule za pemba zilikuwa zinaongoza kwa matokea mazuri , kwa hapa unguja lumumba ilikuwa kiboko ya watanganyika , lakini yote yamekufa kwa sera potofu za CCM , usimlaumu seifu bure, badala yake tumshukuru kwa kuwa mstari wa mbele kupigania uhuru wa zanzibar ambao mungu akijalia hauko mbali.
    Hamumlaumu kikwete ambae amekuwa masuala ya nchi nyengine kama drc , rwanda ameyapa kipa umbele kuwatafutia amani, huku kwetu anatunyonya , anajifanya shujaa kwa wengine , lakini kwake hakuna uadilifu, hakika kama haukutoa uhuru mara hii , ahakikishe hivo vifaru na ndege akaongeze kwani itamwagika damu isiopata kusikilikana , uamuzi anao yeye kama antaka mambo yaamuliwe kwa amani au kwa vurugu.

    ReplyDelete
  6. @Mchangiaji wa 1, 2, na 3..

    nyinyi hamujui mtu anechochea?... Sio ni Huyu Balozi wenu wa Tanganyika Anaeishi Nchini Zanzibar.. Balozi Seif Ali Iddi (jina wala halifanani na vitendo vyake)...

    Tunazo video za CCM You Tube walipofanya Mkutano wakuwatisha Wazanzibari ambao wanataka Muungano wa Mkataba.. Baada ya Mkutano, Watu walianza kuuliwa, Makanisa kuchomwa n.k

    Halafu unasema Seifu Sharifu anachochea.. Nyinyi ndio Ummun Bukmun .. Hivo kusema kwamba Wazanzibari wanahaki ya kudai Nchi yao yenye Mamlaka kamili ndio Imekua Uchocheoo?..

    Washenzi wakubwa nyinyi... Halafu munasema Ati angesomesha watoto wa Form 6... Kwani hamujui kama Elimu ya Zanzibar imeuliwa na hao Wana Mapinduzi wanaochukia Wapemba?

    Niwalimu wangapi wa Kipemba wamehama na kuhamia Tanganyika.. Huko Tanganyika walipofika Walianza na kuuza Maji ya Miwa.. Na wakaendelea mpaka wakatajirika..

    Kwataarifa yenu kama Muungano utavunjika basi hakuna atakaekatazwa kusafiri na kuhamia Tanganyika.. Ikiwa Watu wanahamia Ulaya na ku invest watashindwa kuhamia Udongini kwenu..

    Tafuteni Vitabu musome huko Washenzi nyinyi... I think to be in abroad will teach you a lesson of freedom of speach and Civic Rights.. But its seems to me that, you are still have an empty brain.. Washamba..

    ReplyDelete
  7. Serekali inawajibu hatukatai lakini tujiulize serekali ni nani,hata hao wafanya biashara utajiri wao wamehili kutoka hiyo serekali wasoijua,huyu Malm yeye ndie aliyekiua chuo cha bahari na uvuvi lumumba na kuifafanya secondari,na wakatialipokuwa waziri wa elim aliwapendelea wapemba wenziwe.Mh, Jumbe alitaka siku nyingi sisi tupumue wao wakajipendekeza tanganyika, sasa hakuna nkataba wala uamsho hatutoi ng"o bona nkataba wa unguja na pemba hamuulizi,balahau sidanganye watu,ulikuwa unajicha stalaight,unakimbia wahadim wakikutiya vishindo umesau au ving'o vinakutia batra?

    ReplyDelete
  8. Wapemba msituchanganye sisi Waunguja. Mnachokitafuta tunajua ni madaraka sio kweli kama mnatetea dola ya Zanzibar. Wakati wa utawala wa Jumbe aliyetaka serikali tatu babu yenu huyu seif ndiye aliyekwenda bara kutoa siri hiyo. Sababu alitaka madaraka. Hizo kelele zenu mjue kuwa sisi Wahadimu tumacho. Mnachotafuta madaraka si chengine chochote lakini Unguja yetu hatutoi ngo.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.