Habari za Punde

Mchakato ujenzi Mao Tse Tung

 Khamisuu Abdallah na Ahmed Sakrani (OUT)
TIMU ya wataalamu wanane kutoka nchini China, imewasili Zanzibar kuukagua uwanja wa Mao Tse Tung kwa nia ya kuufanyia matengenezo makubwa.

Akizungumza na wajumbe wa timu hiyo ofisini kwake jana, Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk, amewaomba wataalamu hao kuishawishi serikali ya nchi yao kuufanyia marekebisho uwanja huo ili kulihuisha jina la kiongozi wa zamani wa China Mao Tse Tung.

Waziri huyo alisema, uwanja huo utasaidia kuleta maendeleo ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni pamoja na kukuza mahusiano yaliyopo baina ya Zanzibar na China.

Aidha aliishauri timu ya wataalamu hao kutengeneza ukumbi kwa ajili ya watu mashuhuri (VIP), uwanja wa mpira wa kikapu, ukumbi wa mikutano, michezo midogo, sehemu ya kuegesha magari pamoja na majukwaa ya watazamaji.

Naye mtaalamu Zhang R2, ameahidi kuzungumza na serikali ya nchi yake, kwa lengo la kuufanyia matengenezo uwanja huo.

Aidha amesema baada ya makubaliano kati ya serikali hizo mbili, China itatuma wataalamu wengine kwa ajili ya kuandaa michoro kabla kuanza kwa kazi za ujenzi.

Ujio huo wa wataalamu kutoka China, unafuatia maombi yaliyopelekwa na serikali ya Zanzibar kwa Jamhuri ya Watu wa China, kutaka uwanja huo wenye historia kubwa, ufanyiwe matengenezo.

2 comments:

  1. Kama kuna uwamuzi mzuri SMZ kuwahi kuufanya ktk miaka ya karibuni, basi itakua ni kuufanyia matengenezo uwanja wa maotsetung.

    Huu uwanja umesahaulika siku nyingi na kuna hatari baahi ya wadau wakajikatia viwanja ktk maeneo yanayouzunguka.

    Nilikatiza maeneo yale, miaka miwili iliyopita nilishangaa kuona pale baina ya ukumbi wa AECROTERNAL na UWANJA WA MAU palipokua na mitimti pamesafishwa, sijui alishapewa mwana mapinduzi au ilikua ni project ya serikali?

    ReplyDelete














  2. Kama kweli wata utengeneza itakuwa jambo la maana na wala wasiuite uwanja wa mausting, wa urudishie jina lake la asili ili iwe kivutio kwa watalii, uyo mau kwa sasa siishu, hana msada kwetu sisi waznzibar. Uitwe jina lake la asili na ukarabatiwe uwekivutio kuliko kungoje huruma ya walimwengu








    k

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.