Meneja wa Baraza la Habari Zanzibar Mwenyekiti wa Kikao hicho Suleiman Seif akitowa maelezo ya Mkutano huo wa Baraza la Katiba Tasnia ya Habari Tanzania, uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Manzsons Hoteli Shangani Zanzibar na kuwashirikisha Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania MCT Kajubi Mukajanga, akitowa maelezo ya Rasimi ya Katiba Mpya, Uchambuzi wa Ibara za Rasimu ya Katiba Mpya zinazohusu Haki ya kupata Habari, Uhuru wa Vyombo vya Habari na Haki ya Kujieleza, uliowashirikisha Waandishi wa habari wa Zanzibar.
Meneja wa Udhibiti wa Viwango Baraza la Habari Tamzania MCT Pili Mtambalike, akitowa maelezo ya Rasimu ya Katiba Mpya Mapungufu kwenye Rasimi na Mapendekezo ya Wadau.wakati wa Baraza la Katiba la Tasnia ya Habari kanda ya Kaskazini -Zanzibar kupitia na kutowa mapendekezo yao katika Rasimu hiyo.
Waandishi wahabari wakifuatilia Mjadala wa Rasimu ya Katiba Mpya katika Mkutano wa Baraza la Katiba ulioandaliwa na Baraza la Habari Tanzania.
Waandishi wakisoma Rasimu ya Katiba Mpya wakati wa Mkutano ulioandaliwa na Baraza la Habari Tanzania kwa Waandishi wa habari kuchangia mapungufu yalioko katika Rasimu hiyo.
Mdau wa habari akichangia Rasimu hiyo.
Mdau akichangia Rasimu ya Katiba Mpya wakati wa Mkutano wa Kwanza wa Baraza la Katiba la Tasnia ya Habari Tanzania.
Mchango ukiwasilishwa katika Baraza la Katiba ya Tasnia ya Habari Tanzania Kanda ya Kaskazini -Zanzibar.
Mwandishi Mkongwe wa Habari Zanzibar akichangia katika Mkutano wa Baraza la Tasnia ya Habari Kanda ya Kaskazini -Zanzibar , uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Mazsons
tunaomba video yake tupate kusikia yalozungumzwa ili nasi tujifunze masuala ya katiba.
ReplyDelete