Na Himid Choko, BLW
Katibu
wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Ndugu Yahya Khamis Hamadi amewataka
Wajumbe wa Baraza hilo kutimiza wajibu wao wa kikatiba kwa kuidhibiti Serikali ili kuendeleza uwajibikaji.
Amesema hatua hiyo itafikiwa kwa
kuihoji kuhusiana na sera ,
mipango maalum ya kibajeti pamoja na
kuiuliza masuala mbali mbali yanayohusu
uendeshaji , utekelezaji na usimamizi wa shughuli zake.
Ndugu
Yahaya amesema hayo leo Wakati akitoa mada
kuhusiana na Dhana ya Baraza la Wawakilishi katika kuisimamia serikali iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa
Baraza hilo Mbweni kwenye semina ya siku moja iliyowashirikisha wajumbe
wa Baraza hilo.
Amesema Kanuni za Baraza hilo zimeelekeza wazi Utaratibu wa Mawaziri kuulizwa maswali kuhusu jambo lolote la Umma au jambo
jengine ambalo linasimamiwa na wizara zao. Amesema Mjumbe pia anaweza kuuliza
suala Kwa jambo ambalo Baraza limemteuwa kulishughulikia .
Amesema
serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni serikali ya wananchi, hivyo wananchi hao
kupitia wawakilishi wao waliowatuma kuwawakilish wana haki ya kupata taarifa juu ya mambo
yanavyoendeshwa katika serikali yao .
Katibu
huyo wa Baraza la Wawakilishi amezitaja mbinu nyengine za kuidhibiti serikali kua
ni pamoja na utungaji wa Sheria ambazo itazifuata katika utendaji wa shughuli na mwenendo wake.
Amesema hatua hii ya utungaji wa sheria itasaidia kwa
mtu au kikundi chochote cha watu kuweza
kwenda mahakamani kupinga kitendo au
uamuzi uliofanywa na serikali kinyume na
sheria.
Ameongeza
kufahamisha kwamba njia nyengine ya kudhibiti
utendaji wa serikali ni uidhinishaji wa Bajeti kwa sababu idhini ya Baraza inahitajika ili
serikali iweze kutumia fedha za wananchi katika kutekeleza mipango yake.
“
Endapo Baraza halikuridhishwa na mpango
fulani unaokusudiwa kutekelezwa na serikali au halikuridhika na fedha
zilizoombwa kwa ajili ya kutekeleza mpango huo , basi linaweza kuukataa mpango
huo “ Alisisitiza ndugu Yahya.
Hata
hivyo Katibu huyo wa Baraza la Wawakiklishi amesema kwa namna Baraza hilo
linavyofanya kazi hivi sasa na bila ya Wajumbe wake kujidhatiti, basi serikali itachukua muda kurekebisha
baadhi ya Mapungufu yanayoibuliwa na Baraza hilo na kufanyakazi bila ya
kusimamiwa.
Amewataka
wajumbe hao kufanya kazi zao kwa umakini mkubwa
hasa wanapokua katika Shughuli za Baraza na Kamati zake ili kulinda hadhi na heshima kubwa ya chombo
hicho.
Kwa
upande wa wajumbe hao wameelezea wasi wasi
wao mkubwa hasa kwa Utaratibu wa hivi sasa wa kupitisha kwanza
Bajeti ya serikali kuu na kufutiwa na
bajeti za kisekta.
Wamesema Utaratibu huo unawafanya kukosa nguvu za kuhoji au kuikataa Bajeti za Kisekta kwa vike
inakuwa tayari zimeshapitishwa katika bajeti kuu.
Kwa
upande wake Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais , Ikuli Mheshimiwa Dr. Mwinyi Haji
Mwadini amesema Serikali imekuwa
ikichukua hatua mbali kutokana
na Ripoti au maagizo mbali mbali
yayotolewa na Baraza la Wawakilishi.
Akitowa
mfano Dr. Mwinyi Haji amesema katika Ripoti ya Baraza la Wawakilishi
inayotokana na Kulichunnguza Shirika la Umeme la Zanzibar (ZECO ) na
Baraza la Manispaa Serikali iliwaita wahusika wakuu na kuwahoji pamoja na kuchukua hatua mbai
mbali kwa waliobainika na na kasoro
mbali mbali.
Semina
hiyo iliyofunguliwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mheshimiwa Pandu Ameir
Kificho imedhaminiwa na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP
chini ya |mapango wake wa Kusaidia Mabunge na Vyombo vya Kutunga sheria.
No comments:
Post a Comment