CHAMA cha Mapinduzi, kimesema kitaendelea kutetea
msimamo wake wa mfumo wa muungano wa serikali mbili, utaofanyiwa marekebisho.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye,aliyasema
hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari, mjini Dodoma .
Alisema katika kikao hicho ambacho kilimalizika
juzi usiku wa saa 8:00 chini ya Mwenyekiti wake, Jakaya Kikwete, wajumbe hao
waliamua kuendelea kutetea mfumo huo ambo utakuwa na marekebisho katika vifungu
vilivyopendekezwa na rasimu pili ya katiba.
Alisema nyingi ya chanagmoto ziliomo ndani ya
rasimu hiyo zimepatiwa majibu ambapo kwa
upande wa Tanzania zilikuwa
nane na Zanzibar
tisa.
Alisema
marekebisho waliyopendekeza yatakuwa jibu tosha kumaliza kero za muungano
ziliopo sasa.
Alisema hoja za baadhi ya vya vya upinzani kudai
CCM ina mpango wa kuwaburuza kwa kuwalazimisha kufuata muungano wa serikali
mbili, hazina msingi kwani kila kitu kiko wazi na kinaweza kugeuka ikiwa
kitazingatia nguvu ya hoja.
Alisema
CCM, inawataka wajumbe wa bunge la katika kuwa wazi kujadili rasimu hiyo.
Alisema huu si wakati wa kutishana kwani kuna
mambo ambayo ni muhimu na yanaweza kufanyiwa kazi na kwamba jambo la muhimu ni
kujenga hoja.
No comments:
Post a Comment