Na Rose Chapewa, MBEYA
MWANAMKE mmoja mkazi wa kijiji cha Upendo mkoani
Mbeya Maria Mwamangu (56) ameuawa kwa kunyongwa na kisha mwili wake kutelekezwa
chumbani mwake.
Kabla ya kunyongwa, mwanamke huyo aliharibiwa
vibaya sehemu za siri kwa kubakwa na watu wasiojulikana.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Robert
Mayala alisema tukio limetokea usiku wa kuamkia jana na mwili wa marehemu
ulikutwa jana mchana.
Katika tukio jengine mahabusu aliyefahamika kwa jina
la Vumi Elias (30) mkazi wa Maporomoko Tunduma,
amefariki baada ya kujinyonga akiwa rumande ya polisi wilaya ya Momba.
Kamanada Mayala, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 12:00 asubuhi katika
mahabusu ya polisi ya Tunduma.
Alisema, marehemu alipoteza maisha muda mfupi
baada ya kufikishwa kituo cha afya cha Tunduma.
Alisema marehemu aliingia choo cha mahabusu
majira ya saa nne za usiku na kujinyonga kwa kutumia tambara la kupigia deki.
Alisema taarifa za kujinyonga ziliripotiwa na
mahabusu wenzake waliokwenda chooni kujisaidia ambao walitoa taarifa kwa askari wa zamu.
Alisema, askari hao walikimbia kwa kasi chooni na
kumkuta mtuhumiwa akiwa amejinyonga ingawa bado alikuwa hajafariki.
Alisema, askari hao walimchukua marehemu
akiwa hali mbaya na kumkimbiza kituo cha
afya cha Tunduma ambapo alipoteza maisha wakati akipatiwa matibabu.
Kamanda huyo, alisema marehemu alikuwa akikabiliwa
na kosa la unyang'anyi wa kutumia nguvu na kwamba chanzo cha kujinyonga bado
kinachunguzwa, mwili wake umehifadhiwa chumba cha maiti.
Wakati huo huo, mwanamme mmoja aliyefahamika kwa
jina la Innocent Ndandala, amefariki dunia papo hapo baada ya kupigwa na radi
wakati akichota maji ya mvua wilayani Mbeya.
Akielezea tukio hilo, Mwenyekiti wa kijiji cha
Mpakani, Thabit Mwachura, alisema marehemu alikutwa na mauti wakati akichota
maji ya mvua kwa matumizi ya nyumbani ili kumsaidia mkewe ambae ni mjamzito.
Alisema wakati radi ikipiga marehemu alikuwa
ameshika simu mkononi aliyoitumia kutoa mwangaza.
"Mvua ilikuwa inanyesha, marehemu
alikuwa ameshika simu ya tochi anamuRika
huku akiwa anakinga maji ya mvua, ndiyo radi ikapimpiga na akafariki papo
hapo," alisema.
Alisema tukio hilo lilitokea Februali 16 mwaka huu saa 9:00
alfajiri katika eneo la majengo kijiji cha mpakani Mbarali.
Aidha alisema baada ya kutokea tukio hilo alitoa tarifa kituo
kidogo cha polisi Tunduma wilaya ambapo polisi walifika wakiwa na daktari na
kuthibitisha kifo chake.
Alisema baada ya taratibu za kidaktari kumalizika
mwili ulikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya maziko.
No comments:
Post a Comment