Na Muona Mbali
Nakumbuka Mh. Rais wa Muungano Jakaya Mrisho Kikwete alipotoa tangazo la mualiko kwa Taasisi gani zipeleke majina ya watu kuingia katika Bunge la katiba, aliyataja makundi 10 tu hayakuzidi.
Kuzuka kundi lisiloalikwa na likachaguliwa basi ni nje ya utaratibu alioutangaza awali Mheshimiwa Rais. Ima alikuwa aongezee kwa kulitangaza kundi hilo au kufuta kulitangaza au kufuta kuliteuwa.
Jana yalipotoka majina ya walioteuliwa, limejitokeza kundi la "mapendekezo binafsi", hili pia halikuwemo.Na kinachosikitisha zaidi kateuwa watu 118 na wote ni kutoka Bara. Jee wako wapi Wazanzibari?. Jee hapa haki imetendeka?
Mimi muona mbali naona pameteuliwa kiupendeleo ili kujaza nafasi tu kama ni hadaa.Hivi kama kundi hili la watu kujipendekeza binafsi kama lingelitangazwa jee wazanzibari wasingelijitokeza?
Mimi nahisi ima Raisi alifute kundi hili au aliweke lakini ajaze idadi alau nusu kutoka Zanzibar.
ujumbe wangu kwa wale waznz waliochaguliwa kama sio vibaraka , basi watambue sisi tulisema hatutaki muungano , na kama utakuwepo basi uwe wa mkataba , nashangaa ktk tume ya katiba wanasheria wetu walikaa kimya vipi akina saleh , asaa na awadh wakati mambo ya serikali tatu yanapendekezwa walikuwa wamelala? hicho sicho tulichosema hatutaki mbili wala tatu , tunachotaka ni uhuru kamili au mlileweshwa na sitting allowance mkaka kimya ..funika.... apite.....
ReplyDeleteMkuu habari kama hii ambayo haina ukweli na inayoonesha kuwa muandishi si mtu makini, usingekuwa unaiweka kwa maandishi manene. huyu jamaa anasema Kikwete kateua watu 118 wote wanatoka bara. Hii si kweli jadweli linaonesha wazi kuwa watu 118 kutoka bara walijipendekeza wenyewe na ilikuwa ni kinyume na taratibu kwahiyo hakuna kati yao alieteuliwa. Nakumbuka lile jadweli uliloliweka katika blog yako lilikatika kulia inawezekana ndio maana huyu jamaa hakujua hatima ya hao 118. Lakini alipaswa aangalie sehemu nyengine.
ReplyDeleteJee walioteuliwa kutoka zanzibar chini ya kundi kwa waliojipendekeza kutoka zanzibar ni wakina nani. Wewe unawajuwa.Tutajie.
ReplyDeleteukweli ni kwamba wazanzibari wawe makini,wasipende kupeleka viongozi vivuri wasioweza kutetea hata hoja za wazi kabisa.Kama hakuna uwiano mzuri wa wajumbe basi shughur irudiwe na kwa idadi maalum na wala si kujipendekeza na kisha majina ya wanzanzibari yaachwe.Hii ni danganya toto kwamba mtu anakupa democracy hali anakuua kisaiklojia
ReplyDeleteMsijidanganye wenze3nu hawaku fanya kosa wamechugua vibaraka wao watup, na mtumakini mmja mh, mtikila hao wengine ni matumbo nari hakuna liwalo, fursa tumeipa tukaichezea, chash tujute , watajaza matumboya warudi wana lalamika, kujakuwatia fitina wahadimu wenzao
ReplyDeleteC Mitikila peke yake bwana wee! hata Chunda yuko ng'ang'ari.hahahahahaa .Unajuwa mshikaji ,kikawaida ayakusanyae makumbi huwa na lengo kuyateketeza ama sio!!
ReplyDeleteKatika nchi yenye demokrasia kamili BUNGE lililo bunge la kweli huchaguliwa na watu kwa kupigiwa kura, na sio kusema tu "nafulani ende bungeni" na kama ni kuchaguliwa basi Mansouri anafaa mia juu ya mia lakini kaonekana ni tishio kwa Tanganyika.
ReplyDelete