Na
Mwandishi wetu
KAMISHNA
wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omar Makame, amesema mabomu yaliyoripuka katika
makanisa ya Mkunazini na Kijitoupele na katika mkahawa wa Mercury Forodhani,
hayahusiani na masuala ya kidini, siasa wala utalii.
Aidha
alisema mabomu hayo yametengenezwa kienyeji, ingawa hakuwa tayari kusema
yametengenezwa kwa malighafi gani akisema ingekuwa fundisho kwa wengine kutengeneza.
Alisema
sampuli za mabaki ya mabomu hayo zimechukuliwa kwa uchunguzi zaidi wa
kitaalamu.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Kamishna huyo alisema makachero wenye taaluma ya
kisayansi kutoka makao makuu ya polisi Dar es Salaam wapo Zanzibar kushirikiana na wenzao kufanya
uchunguzi zaidi.
Alisema
hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo, isipokuwa wanamtumia
mtu mmoja ambae atasaidia kupatikana habari kuhusiana na matukio hayo.
Aliwatoa
hofu wageni wanaotaka kuja Zanzibar
akisema nchi ipo katika hali ya amani na usalama na jeshi la polisi litaendelea
kuhakikisha amani inatawala.
Kuhusu
tukio la bomu katika kijiji cha Unguja Ukuu, alisema mmoja kati ya majeruhi
wanne walioripukiwa na bomu, Juma Abdallah, amefariki dunia wakati akipatiwa
matibabu hospitali kuu ya Mnazimmoja.
Alisema
marehemu akiwa na wenzake waliojeruhiwa
na bomu hilo, wakati wakiwa kwa fundi kwa ajili ya kuliyeyusha kutengeneza
nanga ya mashua wakifikiria ni chuma.
Alisema
majeruhi hao ambao ni wavuvi waliokota bomu hilo wakifikiria chuma na kukipeleka kwa
muhunzi kwa ajili ya kutengeneza nanga.
Alisema
tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 6:00 mchana
katika kijiji cha Unguja Ukuu karibu na eneo linalotumiwa na wanajeshi wa Jeshi
la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ) kwa ajili ya mafunzo.
Alisema
baada ya tukio hilo
majeruhi walikimbizwa hospitali ya Mnazimmoja kwa matibabu na ilipofika saa
1:00 usiku mmoja kati ya majeruhi hao alifariki dunia.
Alisema
tayari maiti hiyo imeshakabidhiwa kwa familia yake na kuzikwa jana kijijini
kwao Unguja Ukuu.
Hata
hivyo, aliwataka wananchi endapo wataokota kitu ambacho sio cha kawaida ni
vyema kutoa taarifa kwa jeshi la polisi na kwa viongozi wa shehia ili kuepukana
matatizo.
No comments:
Post a Comment