Na
Khamis Haji OMKR
MAKAMU
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ,
Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amewasihi wabunge wa bunge maalum wanaojadili
rasimu ya pili ya katiba kuweka mbele maslahi ya nchi na kuelewa kuwa Jamhuri
ya Muungano imetokana na nchi mbili zilizokuwa dola huru.
Alisema
hayo wakati akifungua maonesho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
yanayoendelea hadi Aprili 19 katika viwanja vya Mnazimmoja jijini Dar es Salaam .
Alisema
wabunge hao wajielewe kuwa wana wajibu mkubwa kwa Watanzania, lakini pia
wafahamu kwamba kazi yao
kubwa ni kuhakikisha kero za Muungano zilizodumu kwa muda mrefu tokea Muungano
huo ulipoasisiwa miaka 50 iliyopita zinakuwa historia.
“Nawasihi
wabunge waangalie maslahi ya nchi mbili zilizokuwa dola huru, wafahamu kuwa
ziliungana kwa hiari, lazima tusikilize hisia za kila upande na wala tusichukue
maamuzi ya haraka, tukifanya hivyo
tusababishia tusipate katiba iliyo bora,”, alionya.
Alieleza
ipo haja wabunge wajiulize katiba inayotafutwa itatatuaje kero zilizopo, je
itakidhi haja na kukabili changamoto zilizopo, ikiwemo mgogoro wa katiba
ulioelezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Warioba, kati
ya katiba ya Jamhuri na ile ya Zanzibar .
“Nadhani
Warioba alipotoa mapendekezo ya Tume aliona ugumu wa suala hili, lazima hilo lizingatiwe.
Watanzania wanataka Katiba ambayo italeta usawa na nchi mbili zilizoungana
kuheshimiana,” alieleza.
Alisema
huu si wakati wa kikundi fulani kujifanya kina haki zaidi, lazima kila upande usikilizwe
unasemaje, ili baadaye maoni na mawazo tafauti yaweze kupimwa na kufanywa
maamuzi sahihi ambayo yatawezesha kusaidia kupatikana katiba itakayodumu kwa miaka mingi ijayo.
“Tujiepushe
na kikundi kimoja kujifanya kina haki zaidi, sote tuna haki sawa,” alisisitiza
Makamu wa Kwanza wa Rais.
Akitoa
shukurani kwa mgeni rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,
Mohammed Aboud Mohammed, alisema wabunge wa bunge maalum wanaoendelea na
mjadala mjini Dodoma wako makini na watapima kila hoja inayowasilishwa ili
hatimaye waweze kupata katiba iliyo bora.
Naye
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira, Binilith
Mahenge, alisema maonesho hayo ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
ni fursa ya kihistoria kwa wananchi wa Tanzania kwa vile hayajapata
kufanyika kwa miaka 50.
Alisema
wananchi watapata taaluma na taarifa mbalimbali zinazohusu mafaniko na
matarajio ya taasisi mbali mbali za Muungano, pamoja na kupata fursa ya kutoa
maoni yao juu
ya mipango inayotekelezwa.
Mla vitam ,haachi kujiramba.
ReplyDeleteCCM hata waambiwe nini hawawezi kubadilika, wao wapo pale bungeni kwa ajili ya sera ya chama sio kwa ajili ya kujadili na kuifanyia maboresho katika iliyowasilishwa na tume ya Jaji J.Warioba
ReplyDeletemaalim Seif kweli wewe mtu hatari ! kwanini usingesema tuu UKAWA walichofanya ni kitendo cha kuwazalilisha waTanzania walio watuma Dodoma?
ReplyDelete