Habari za Punde

Darajani kumetokea Mlipuko unaosadikiwa kuwa ni Bomu



Kuna taarifa ya kutokea mlipuko na mlio mkubwa mithili ya bomu umetokea maeneo ya Darajani karibu na msikiti na kujeruhi Wahadhiri waliokuwepo katika msikiti wa Darajani mara baada ya kumalizika Sala ya Isha.
 
Mlipuko huo unasemekana umetokea baada gari ambalo lililopita mbio na kurusha kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu kwenye gari ambalo wangelitumia wahadhiri waliokuwa katika Muhaadhara ndani ya Msikiti
 
Kuna taarifa kwamba mtu mmoja mpaka sasa amepoteza maisha.
 
Tukipata taarifa zaidi tutawajuulisha

4 comments:

  1. Innalillahi wainna ilaihi rajiuun

    Allah ampokee mja wake huyo aliyedhulumiwa na amsamehe makosa yake. Amin

    ReplyDelete
  2. Mungu ampe safari njema

    ReplyDelete
  3. hiyo taarifa haijapatikana hadi leo?

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.