Habari za Punde

Kijana Mwanaid Vuai Saleh Akiwa Wodini Hospitali ya Jeshi Bububu.

Akaunti ya Kumchangia Kijana Mwanaid Vuai Saleh (26)
A/C 051206007686
Tawi la PBZ Malindi 
Zanzibar.
Kijana. Mwanaid Vuai Saleh,  mwenye umri wa miaka (26), Mkaazi wa Chumbuni Wilaya ya Mjini  Zanzibar, ambaye amapata ajali ya moto akiwa katika kazi za nyumbani. 

Amaomba msaada kwa ajili ya kupata matibabu nje ya Nchini India, ili kupata matibabu zaidi ili kuweza kurejesha hali yake, Gharama ya matibabu yake inahitajika Shilingi Milioni 15, kuweza kumsafirisha nchini India. ilimkupata matibabu . Kwa sasa yuko katika hospitali ya Jeshi Bububu anaendelea na Matibabu hayo akisubiri misaada ya Wasamaria wema ili kumuwezesha kupata Fedha kwa ajili ya matibabu yake nchini India.

 Kwa Mwananchi yoyote mwenye msaada wake anaweza kutumiza Akaunti ya Benk katika Tawi la Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ ) Tawi la Malindi A/C 051206007686. Kwa misaada zaidi  unaweza kufika hospitali ya Jeshi Bububu . Unaweza kuwasiliana na Mama yake Mzazi Bi Jina Haji Khamis, anapatikana kwa kuwasiliana kwa No hii. 0773 569466, anakaa na Mwanaidi Hospitalini hapo.Bububu Jeshini.  

Kwa maelezo Zaidi unaweza kuwasiliana na Ndugu wa Mwanaidi 
Ali Mkali  kwa hiyo No0777 469345
Pavu Omar NO 0779 485306
Pia unaweza kuwasiliana na Mdau wa Blog Hii Othman MaulidNo 0777424152.
Mzazi wa Kijana Mwanaid Vuai Saleh, Bi Jina Haji Khamis, akizungumza mkasa wa Mtoto wake kwa masikitiko makubwa na Mdau wa Blog hii ya Zanzinews.com, alipofika kumtembelea Mwanaid kuona hali yake halisi baada ya kupata ajali hiyo. Na kusema sasa ni miezi minne anamuuguza Mwanawe, akiwa katika wodi hiyo katika hospitali ya Bububu akisubiri wasamaria wema kupata msaada wa kuweza kumsafirisha mtoto wake kupelekwa India kwa matibabu ya majeraha ya moto. 
 
Amesema matibabu ya motto wake yanahitaji shilingi milioni 15 za kumsafirisha na kupata matibabu..Amesema hivi sasa akiwa hapa hospitali inambidi kutumia shilingi karibu elfu kumi kwa ajili ya dawa zake kila siku inahitajika kubadilishwa dawa. 
 
Anawaomba Wananchi kumsaidia ili kuweza kumsafirisha mtoto wake kupata matibabu nje ya Nchi 
Kijana Mwanaid Vuai Saleh akiwa katika Wodi ya hospitali ya Bububu jeshini akipata matibabu hospitalini hapo akisubiri misaada ya wasamaria ili kuweza kusafirishwa kupata matibabu zaidi. Kwa sasa yuko hospitalini miezi Minne akisubiri Fedha kupitia kwa Wasamaria kumchangia na ndugu na jamaa wanahangaika kupita kila upande kuomba misaada kuweza kumsaidia nguyu yao..Mwanaid Vuai Saleh. Tayari ameshapoteza jicho moja la upande wa kulia na jicho la kushoto likiwa linaoha linahitaji matibabu ya haraka ili kuweza kuliokoa kwa sasa linaona linahitaji tiba.kama linavyoonekana   



Mama wa Mwanaid Bi Jina akionesha mkono wa mtotio wake ukiwa umepata ulemavu kwa kupoteza vidole vyake katika ajali hiyo ya moto.


2 comments:

  1. Inna llaaha maa swaabiryna. Kwanza tunawaomba wazee na kijana Mwanaidi kuwa na subira na mitihani ya Allah. Hayo ni katika majaribu ya Allah, tustahamili na tuwe na subra na jaza yake iko kwa Allah, Allah ni muweza wa kila kitu na inshaallah kwa rehma zake atampa uzima wa haraka amiin.

    Pamoja na hayo , kitu kimoja kimenigusa pia naomba nikizungumze. Hii picha kwa uoni wangu haikustahiki kupigwa hivyo ilivyopigwa. ILipaswa kuonesha sehemu tu zile zilizoathirika. Sehemu ya kichwa pekee ilitosha kutoa picha halisi ya mtihani aliopata ndugu yetu Mwanaidi. Haikustahiki kuonesha sehemu za kifua, hasa tukizingatia kwamba muathirika ni Mwanamke tena wa kiislam ambapo sehemu hizo ni "aura" zinapaswa kustiriwa. Imekuwa kwa kiasi fulani kama kumkashifu pamoja na kwamba lengo lilikuwa kufikisha ujumbe wa kutaka kumsaidia.

    Ushauri wangu kwa kaka yangu Ndugu Othman, (nikiamini ni mwanahabari makini mwenye kuelewa maadili ya kazi yake) kuzifanyia ''editing'' hizi picha ili kuonesha sehemu stahiki tuu, ingawa najua tayari zimeshasambaa sehemu nyingi lakini bora kufanya hivyo kuliko kuachia kabisa kwani jukumu pia litakuangukia.
    Wabillaah tawfiiq

    ReplyDelete
  2. Shukran mdau kwa ushauri na angalizo. tayari tumeshazifanyia editing. Pia tunawaomba radhi wadau kwa kosa lililofanyika nia na dhamira ilikuwa kuona hali halisi lakni pia tunatakiwa kuchunga maadili ya kazi zetu, utamaduni wetu pamoja na dini yetu pia.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.