Na Halima Jumbe
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya
ya magharibi Unguja,imesema haitasita kumchukulia hatua mwananchi yeyote
atakaebainika kuvunja sheria kwa ajili ya maslahi yake binafsi.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mkuu
wa wilaya hiyo, Ayoub Mohammed, alieleza hayo
katika ziara maalum iliyofanywa na wajumbe wa kamati hiyo katika shehia
za Kombeni, Nyamanzi, Chukwani na Kiembesamaki kwa ajili ya kuangalia maeneo
yanayolalamikiwa na wananchi.
Akizungumza na wawanchi hao kwa
nyakati tofauti,alisema serikali imeweka mipango madhabuti kwa kila sekta ili kuhakikisha wananchi
wanazitumia furasa zilizopo kwa mujibu wa sheria na kudumisha amani na utulivu.
“Sheria zilizopo zinafaa
kutekelezwa na kila mwananchi, hazibagui mkubwa wala mdogo au mwenye cheo na
asiye na cheo kila mmoja anapaswa kuziheshimu na uongozi wa wilaya utahakikisha
unalisimamia jambo hilo,”alisema.
Wakizungumza na wananchi wa
shehia za Kombeni na Dimani, wajumbe hao walipokea malalamiko ya kuwepo
uharibifu wa mazingira katika eneo la kihistoria la hifadhi ya mikoko Dimani.
Ofisa kutoka idara ya misitu na
mali zisizorejesheka, Mwinyi Juma Muharram, alisema taasisi yake imeanza
kuyafanyia kazi malalamiko hayo kwa lengo la kuendeleza historia hiyo
isitoweke.
Malalmiko mengine ni kuhusiana
na ujenzi wa uzio wa ukuta kwenye shamba la Mohammed Hashim na kusababisha kuziba
njia za asili zinazotumiwa na wananchi.
Nae Mwenyekiti wa kamati hiyo,
aliwaahidi wananchi hao kufanya mazungumzo ya pamoja kati ya mlalamikiwa na walalamikaji na
kumtaka sheha wa shehia hiyo kusimamia
na kuhakikisha mivutano ya aina hiyo haiendelei tena.
Aidha kamati hiyo pia
ilitembelea diko la Dimani
linalolalamikiwa kutumika kama bandari
bubu ya kusafirishia bidhaa za magendo zikiwemo dawa ya kulevya na bangi.
Wakitoa malalamiko yao wavuvi
wa eneo hilo walidai bidhaa hizo hupitishwa katika bandari hiyo kwa kutumia
gari.
Wakiwa katika eneo hilo wajumbe walifanikiwa kumkamata kijana Salmini Khamis (20)
mkaazi wa Nyamanzi, akiwa katika harakati za kutaka kusafirisha vipolo 6 vya
sukari na sabauni kipolo 1 kwa njia ya
mgendo na kumfikisha katika kituo cha polisi Mazizini.
Hata hivyo, kamati hiyo
iliwataka wavuvi kutoa ushirikiano kwa
vikosi vya ulinzi na usalama kwa kutoa taarifa watakapowabaini watu
wanaojishughulisha na vitendo viovu.
Kamati hiyo pia ilitembelea
soko la samaki la Mazizini na kumuagiza Mwenyekiti
wa wavuvi na madalali,Faki Haji Makame, kuorodhesha majina ya wavuvi ili wasajiliwe.
Maeneo mengine waliyotembelea ni eneo la machinjio
ya ngo’mbe Kisakasaka lenye ukumbwa wa ekari 100 lilovamiwa na wananchi kwa
ajili ya ujenzi wa nyumba za makaazi

Ni mwanzo mwema kwa Mkuu Wa Wilaya mpya ndugu Ayoub, naamini atakuwa mwadilifu katika kazi zake name Allah ampe wepesi katika kufanikisha majukumu take kwa maslahi ya wananchi wote. Ila paragraph ya mwisho haikunirahisha. Suala la wananchi Eti kuvamia maeneo, hoi so sahihi ukisema wananchi kuvamia maeneo na kujenga makaazi, suala langu hivi kwani serikali imetenga maeneo maalum yaliyopimwa au yanayokubalika kwa Ujenzi Wa makaazi Wa wananchi hasa wanyonge?? Mh. Ayoub nakuamini sana kwa utendaji wako kwani nakuelewa mila nakuomba sana kwa vile sasa una nafasi nzuri kuhakikisha wanyonge wanapata maeneo yaliyopimwa name serikali kea ajuli ya majenzi. Vyenginevyo matatizo munayoyaita uvamizi Wa maeneo hayataisha milele. Nakutakia kazi njema name uadilifu. Amiin
ReplyDelete