Na Mwanajuma Mmanga
Jumla ya miradi 19 yenye
thamani ya dola za Marekani 236 milioni imewekezwa kuanzia Januari hadi Oktoba 2014.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka
ya Uimarishaji Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA), Salum Khamis Nassor, alisema hayo
wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake Maruhubi.
Alisema miradi hiyo ni pamoja
na ya sekta ya biashara, hoteli ya mikahawa, huduma, afya na utembezaji wageni na michezo ya baharini.
Alisema katika sekta ya biashara
miradi miwili yenye thamani ya dola 22,319,758 imesajiliwa, hoteli na mikahawa
miradi 7 yenye thamani ya dola 52,031,235 na huduma miradi 6 yenye thamani ya
dola 160,780,000.
Miradi mengine ni ya afya mradi mmoja wenye thamani ya dola
1,275,000 na mradi mmoja wa watembeza wageni na michezo ya baharini wenye
thamani ya dola 500,000.
Alisema miradi hiyo imeanzishwa
kutokana na Zanzibar kuwa mazingira mazuri ya uwekezaji yanayowavutia
wawekezaji wengi.
Alisema majukumu ya ZIPA ni
pamoja na kurahisisha na kuwasaidia wawekezaji kupata vibali, kuwaunganisha,
kutafuta taarifa kwa ajili ya wawekezaji na wafanyabishara na kutatua
changamoto zinazojitokeza katika uwekezaji.
Aliwataka wawekezaji kufuata masharti
na taratibu zilizowekwa na mamlaka hiyo ili kuepuka usumbufu usio wa lazima.

No comments:
Post a Comment