Na Zuhura Juma, Pemba
Wakazi wa kisiwa cha Uvinje wilaya
ya Wete mkoa wa kaskazini Pemba, wamemuomba Mwakilishi wa jimbo la Gando, Mhe. Said Ali Mbarouk, kuzuia
ujenzi wa hoteli katika kisiwa hicho, kwa hofu kwamba inaweza kuwa chanzo cha
kuharibu mila, utamaduni na silka ya vijana wao.
Walisema hayo wakati
walipokutana na Mwakilishi huyo ambae pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni,
Utalii na Michezo hivi karibuni.
Mmoja wa wakazi hao Biwanu Ali
Ussi, alisema utalii unaweza kusababisha vijana wao, hivyo hawako tayari
kupokea mradi huo.
“Mimi binafsi nimeshuhudia hali hii, watalii
wanapofika tu hapa, darasani wanafunzi wote hukimbia, kwa sababu wanawapa fedha
na hili ni tatizo,” alisema mwakijiji
huyo ambae pia ni mwalimu.
Simai Ali Simai (Karambisi)
ambaye nae anaishi kisiwani hapo, alisema wameanza kupata hofu ya utalii kwa
sababu wana hakika vijana wao wataharibika.
“Leo hii hawajajenga wanatembea tu watoto wote
wanakimbia skuli, majumbani na kuwafuata, je wakijenga hoteli watalii wakaja
kwa wingi watasoma tena, si watarejea ajira za watoto zinazokataliwa?,”
alihoji.
Kwa upande wake Mwakilishi wa
jimbo hilo, aliwataka wananchi hao kupunguza jazba na kukaa kwa amani, kwani
kinyume na hivyo wanaweza kutofautiana miongoni mwao akisema lengo la serikali
ni kuimarisha sera ya utalii kwa wote.
Aliwaahidi wakazi wa kisiwa
hicho kwamba atawapeleka ngazi zote za serikali zinazohusika na shughuli hizo,
ikiwa ni pamoja na Mkuu wa mkoa huo, Mkuu wa wilaya, Kamisheni ya Utalii,
Mamlaka ya ardhi pamoja na Mamlaka ya Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA), ili kuwasilisha
malalamiko yao.
No comments:
Post a Comment