Habari za Punde

Waumini wa Dini ya Kikristo Zanzibar Wajumuika katika Ibada ya Krismas.

Farther Charles Lundu akiendesha Ibada ya Krismas , kwa lugha ya kiingereza katika Kanisa la Anglikana Mkunazini  iliohudhuriwa na waumini mbali mbali kutoka nje ya Zanzibar wakiwa katika matembezi yao na kuhudhuria Ibada hiyo. iliofanyika katika kanisa hilo leo asubuhi.
Waumini wakiwa katika Ibada ya Krismas katika Kanisa la Anglikana Mkunazini Zanzibar, wakijumuika na waumini wengine duniani kuadhim isha kuzaliwa kwa Yesu.
Waumini wakiwa katika Ibada ya Krismas katika Kanisa la Anglikana Mkunazini Zanzibar, wakijumuika na waumini wengine duniani kuadhim isha kuzaliwa kwa Yesu.
 Waumini wa Kanisa la Anglikana Mkunazini wakiwa katika Ibada ya Krismas leo asubuhi kuadhimisha kwa kuzaliwa Yesu..
 Waumini wa Kanisa la Anglikana Mkunazini Zanzibar wakipeana mkono wa kheri baada ya kumaliza Ibada ya Krismas ilioendeshwa kwa lugha ya kiingereza na Farther Charles Lundu, ikiwa ni maadhimisho ya kuzaliwa kwa Yesu. 
 Farther Charles Lundu akiwasalimia waumini na kupeana mkono wa kheri baada ya kuadhimisha Ibada ya Krismas katika Kanisa la Mkunazini Zanzibar, wakiungana na Waumini wa madhehebu mbalimbali Duniani kuadhimishi siku hii 
Mchungaji Filipo Mvungi akiongoza Ibada ya Krismas kwa kuadhimisha kuzaliwa kwa Yesu, iliofanyika katika Kanisa hilo la KKKT Mwanakwerekwe Dayosisi ya Zanzibar na kuhudhuriwa na waumini wa kanisa hilo ikiwa ni kuadhimisha siku hiyo ya kuzaliwa  kwa Yesu.
WAUMINI wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Zanzibar  Mwanakwerekwe Unguja wakiwa katika Ibada ya Krismas iliongozwa na Mchungaki Filipo Mvungi na kuungana na waumini wa madhehebu mbalimbali ya kikristo duniani katika kuadhimishi siku ya kuzaliwa kwa Yesu.
WAZIRI Mkuu Mstaaf Mhe Edward Lowasa, akijumuika na waumini wa Kikristo wa kanisa la KKKT Mwanakwerekwe Zanzibar katika Ibada ya Krismas, ilioongozwa na Mchungali Filipo Mvungi, iliofanyika katika kanisa hilo,na kuungana na waumini wa dini ya Kikristo duniani kuadhimisha siku hiyo ya krismas
Waziri Mkuu Mstaaf Mhe Edward Lowasa, akitowa nasaha zake kwa waumini wa Kanisa la KKKT Zanzibar baada ya Ibada ya Krismas kumalizika katika kanisa hilo huko mwanakwerekwe Zanzibar. 

Waumini wa Kanisa la KKKT Mwanakwerekwe Zanzibar wakimsikiliza Mhe Lowasa akitowa Salamu za Krismas kwa waumini wa kanisa hilo baada ya Ibada ya Krismas iliofanyika leo asubuhi na kuongozwa na Mchungaji Filipo Mvungi, Mhe Lowasa hujumuika na waumini wa kanisa hilo killa mwaka wakati wa Ibada ya Krismas hufika Zanzibar kuadhimisha.

Waumini wa Kanisa la Tanzania City Christian Center Kariakoo Zanzibar, wakitowa sadaka baada ya kumaliza kwa Ibada ya Krismas iliofanyika katika kanisa hilo kuadhimisha kwa kuzaliwa kwa Yesu Kikristo

Waumini wa Kanisa la Tanzania City Christian Center Kariakoo Zanzibar, wakitowa sadaka baada ya kumaliza kwa Ibada ya Krismas iliofanyika katika kanisa hilo kuadhimisha kwa kuzaliwa kwa Yesu Kikristo

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.