Habari za Punde

Balozi Seif akagua shughuli za uchimbaji wa kisima Muembe Majogoo

 Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi aliyevaa shati rangi ya Kijani akikagua maendeleo ya uchimbaji wa Kisima cha maji safi katika Kijiji cha Muembe Majogoo.
 Wanachama wa CCM na Wananchi wa Kijiji cha Muembe Majogoo wakiwa katika mkutano wa kutathmini suala la huduma za maji safi katika Kijiji chao wao na Mbunge wao Balozi Seif hayupo pichani hapo kwenye Tawi la CCM Muembe Majogoo.
Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kitope Mama Asha Suleiman Iddi akiwapa matumaini ya upatikanaji wa huduma za maji Sadfi na salama wananachi wa Kijiji cha Muembe Majogoo
 
 
Na Othman Khamis Ame, OMPR
 
Uongozi wa Jimbo la Kitope uko katika jitihada za kufanya maarifa ya kuhakikisha huduma za maji safi na salama inapatikana katika kijiji cha Muembe Majogoo ili kuwaondoshea u Wananchi wa Kijiji hicho usumbufu wa ukosefu wa huduma hiyo muhimu.
Mbunge wa Jimbo la Kitope ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wanakati akizungumza na wanachama wa chama cha Mapinduzi pamoja na wananchi wa Muembe Majogoo mara baada ya kukagua shughuli za uchimbaji wa kisima katika kijiji hicho.
Balozi Seif alisema uongozi wa Jimbo hilo unaelewa vyema shida na matatizo yanayowakumba wananchi hao katika kutafuta huduma za maji safi na salama kwa muda mrefu. Hivyo kazi inayoendelea ya uchimaji wa kisima hicho imelenga kukabiliana na tatizo hilo.
Aliwahakikishia wananchi hao wa Kijiji cha Muembe Majogoo kwamba kazi hiyo ya uchimbaji wa  kisima inayoendelea itakwenda sambamba na ununuzi wa mipira ya kusambazia maji katika kijiji hicho.
Aliwapongeza wanachama wa chama cha Mapinduzi na Wananchi wa Kijiji cha Muembe Majogoo kwa ustahamilivu wao wa muda mrefu waliouonyesha katika kipindi choche cha ukosefu wa huduma hiyo muhimu.
Akigusia suala la Kura ya maoni kuhusu Katiba Mpya ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inayopendekezwa pamoja na uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu Balozi Seif alisema Umoja na Amani Nchini Tanzania utadumu endapo Muungano uliopo hivi sasa utaendelea kuwepo.
Balozi Seif alisema wapinzani nchini walikuwa wakipigia kelele uwepo wa mfumo wa Serikali tatu katika Katiba iliyopendekezwa wakiwa na lengo maalum la kutaka kuona Muungano uliopo unavunjika.
Alitahadharisha kwamba huu ni wakati wa fitina kutokana na kukaribia kwenye uchaguzi Mkuu. Hivyo Wana CCM lazima wahakikishe wanaendelea kushikamana na kushirikiana nili Chama cha Mapinduzi kiendelee kuongoza Dola katika chaguzi zote zijazo.
Balozi Seif alisema njia ya kuyakimbia au kukabiliana na fitina hizo ni kwa wanachama hao kuepuka makundi yaliyoanza kujichomoza ya kutaka kuwaunga mkono watu wataoamua kugombea nafasi za Uongozi  wakati muda wa kufanya hivyo bado haujafika wala kutangazwa.
Mapema Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kitope Mama Asha Suleiman Iddi aliwaeleza Wana CCM na Wananchi hao wa Muembe Majogoo kuwa mpango maalum utafanywa wa kusogeza huduma ya umeme katika kijiji hicho ili kurahisisha kazi za usambazaji wa maji safi na salama.
Mama Asha alisema mpango huo unatarajiwa kutekelezwa katika kipindi kifupi kijacho ili ile kiu waliyonayo wananchi hao ya upatikanaji wa huduma za maji safi iweze kufikiwa vyema.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.