Na Mwandishi Wetu
Watuhumiwa wengine watatu
waliokwapua fedha za escrow wamefikishwa katika kizimba cha mahakama ya hakimu
mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kujibu mashtaka ya kupokea rushwa.
Walioshtakiwa ni Mkurugenzi wa fedha
wa benki ya Mkombozi, Julius Ruta, ambae amakosa dhamana, Ofisa Mwandamizi wa
TANESCO, Steve Urasa na Leonard Lutabingwa wa TRA anayeshitakiwa kwa makosa
manne.
Kushtakiwa kwa watendaji hao
kunafanya idadi ya watu walioburuzwa mahakamani kutokana na sakata hilo kufikia
watano.
Wengine ni Rugonzibwa Mujunangoma na Theophillo Bwakea ambao
walifikishwa mahakamai Kisutu, wakikabiliwa na mashitaka ya rushwa baada ya
kupokea mgao wa shilingi milioni 485.1 kutoka kwenye akaunti ya Tegeta Escrow
walizohamishiwa na James Rugemalira.
Katika kesi ya kwanza, aliyekuwa Mwanasheria
wa Mamlaka ya Vizazi na Vifo (Rita) Mujunangoma ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi
wa Sheria Wizara Ardhi, Nyumba Maendeleo ya Makazi, alisomewa mashitaka yake
mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Emmilius Mchauru.
Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Mwendesha Mashitaka
wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai
akisaidiana na Max Ari, ulidaiwa Februari 5, mwaka 2014 katika benki ya
Mkombozi iliyopo Ilala jijini, mshtakiwa akiwa Mkuu wa Sheria wa wizara
hiyo,alipokea rushwa.
Ilidaiwa kuwa mshtakiwa alipokea rushwa ya shilingi
milioni 323.4 kama zawadi kupitia akaunti yake namba 00120102062001 kutoka kwa
Mshauri binafsi wa kimataifa na Mkurugenzi wa zamani wa IPTL,James Rugemalira
baada ya kuwa mjumbe katika menejimenti ya Rita wakati wa machakato wa
kuipitisha IPTL kuiuzia Tanesco umeme.
Katika kesi ya pili, aliyekuwa mjumbe wa
kitengo cha kuidhinisha Tanesco kununua umeme wa IPTL,Wizara ya Nishati na
Madini, Injinia Bwakea kwa sasa mtumishi wa Wakala wa Umeme
Vijijini(REA),alisomewa mashitaka yake mbele ya Hakimu, Frank Moshi.
Ilidaiwa mshtakiwa akiwa Injinia
Mkuu wa REA, alipokea rushwa ya shilingi milioni 161.7 kupitia akaunti namba
00410102643901 ya Tegeta Escrow kama zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Rugemalira.
No comments:
Post a Comment