Habari za Punde

Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa mjini magharibi

 Mlezi wa Mkoa wa Magharibi Unguja Kichama Balozi Seif Ali Iddi akiwapungia Mkono Viongozi wa Mkoa huo Afisi ya           CCM Wilaya ya Dimani hapo Kiembe Samaki wakiwa tayari kuupokea Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana aliyepo Visiwani Zanzibar kwa Ziara ya Kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mlezi wa Mkoa wa Magharibi CCM Balozi Seif Ali Iddi kwenye afisi ya CCM Wilaya ya Dimani hapo Kiem be Samaki kabla ya kuanza ziara yake ndani ya Mkoa huo.
 Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Magharibi wakiwa katika kikao maalum na Katibu Mkuu wa CCM Nd. Abdulrahman Kinana cha kutathmini utekelezaji wa Ilani ya CCM Ndani ya Mkoa huo.
Katibu Mkuu wa CCM Nd. Abdulrahman Kinana akielezea msimamo wa CCM kupinga rushwa wakati akizungumza na Viongozi wa CCM Mkoa wa Magharibi Unguja.
Picha na – OMPR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.