Habari za Punde

Bandamaji Wapata Masjid Mpya

Mwenyekiti wa Kamati ya kuendeleza ujenzi wa Misikiti na Madrasa Zanzibar Rais Mstafu wa Tanzania Al-Hajj Ali Hassan Mwinyi akitoa salamu wakati wa hafla ya ufunguzi wa Msikiti Mpya wa Ijumaa wa Kijiji cha Bandamaji Mvumoni Mkoa wa Kaskazini Unguja.Kulia ya Mzee Mwinyi ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Mfadhili wa Ujen zi wa Msikiti huo Sheikh Muhoma.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu wa Kijiji cha Bandamaji Mvumoni mara baada ya kuufunguwa rasmi Msikiti wa Ijumaa wa Kijiji hicho kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Al-Hajj Dr. Ali Mohammed Shein.
Balozi Seif akigawa Misahafu kwa ajili na Madrasat Taawun na Masjid Bilal wa Kijiji cha Bandamaji Mvumoni mara baadsa ya kuzindua Msikiti na Madrasa hiyo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akibadilishana mawazo na Mke wa Mfadhili wa Ujenzi wa Msikiti Bilal wa Bandamaji Mama Fatma nje ya msikiti huo.Kati kati yao ni Mjumbe wa Baraza la Ulamaa Mkoa wa Kaskazini Unguja Sheikh Khamis Abdulhamid.(Picha na –OMPR )

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.