Na MAELEZO ZANZIBAR 02/04/2015
SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMEKANUSHA TAARIFA ZILIZOTOLEWA NA BAADHI YA VYOMBO VYA HABARI KWAMBA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI WALIIHUSISHA SERIKALI YA OMAN NA UPOTEVU WA NYARAKA ZA SERIKALI.
HAYO YAMEELEZWA NA WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR MOHAMED ABOUD MOHAMED KATIKA TAARIFA YAKE ALIYOITOWA KWA VYOMBO VYA HABARI.
TAARIFA HIYO IMESEMA HAKUNA HATA MJUMBE MMOJA WA BARAZA LA WAWAKILISHI AMBAYE KATIKA MCHANGO WAKE KWENYE BARAZA HILO ALIIHUSISHA SERIKALI YA OMAN NA UPOTEVU HUO.
AIDHA TAARIFA HIYO IMESISITIZA KUWA SERIKALI YA OMAN HAIHUSIKI NA UPOTEVU WA NYARAKA HIZO NA WALA HAIKUMTUMA MTU YEYOTE KUFANYA JAMBO HILO.
TAARIFA HIYO IMEELEZA KUWA OMAN NA ZANZIBAR NI NCHI ZENYE HISTORIA KUBWA NA MASHIRIKIANO MEMA HIVYO SI VYEMA KWA KUTIWA DOSARI KWA TAARIFA ZISIZO SAHIHI ZINAZOTOLEWA NA BAADHI YA VYOMBO VYA HABARI.
TAARIFA HIYO IMESEMA WAJIBU WA VYOMBO VYA HABARI NI KUYAENDELEZA MAHUSIANO MEMA NA MASHIRIKIANO YALIYOPO BAINA YA SERIKALI YA OMAN NA ZANZIBAR
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR
Njaa ni shidaaa, acha blabla tunataka nyaraka zetu.
ReplyDeleteAcha tu ziende ili tupate uchungu!.. Visiwa hivi havina uzalendo hata kidogo! Tulio wengi tunadhani kuzaliwa Z'bar hususan shamba ndio uzalendo wenyewe kln. kumbe sivyo!
ReplyDeleteUzalendo ni zaidi ya hivyo, ni pamoja na kuelewa mali mbali mbali za Z'bar, kizitetea , kuzilinda na kuzitunza.
Leo hii watu wamepata uchungu kwa kusikia upotevu wa nyaraka lkn. hawajiulizi ni mara ngapi ktk historia makumbusho yetu yaliwahi kuvamiwa na kuibiwa vitu mbali mbali!
Wala hawajiulizi ni mali ngapi za namna hiyo zinaendelea kupotea kwa vile tuliowengi hatuna taarifa nazo na hatutaki kujua
Vitu kama vile Targisi na baadhi ya nyaraka zinazohusiana na familia ya muimbaji maarufu wa uingereza FREDY MURCURY nazo zilienda lkn. hakuna anaejali mpaka aje asikie BLW.
Jambo la mwisho ni kuuzwa kwa hekalu la MAPARISI kwa MUZAMMIL pamoja vitu mbali mbali vya kihisotoria! Huu ni uhalifu mkubwa kwa vile majengo ya ibada sio mali ya mtu binafsi!
Kwa mfano leo hii WAANGLIKANA waseme wanauza kanisa lao mkunazini ili lifanywe hoteli hivi serikali itaridhia?
Wakati wa SALMINI mhe RAZA alipita maofisini na kukusanya samani za kale( antiques) na kurudishia samani za fomeka, watu kimyaa kama hawapo!
Pia gari lililoachwa na BRITISH RESIDENT wa mwisho Z'bar kabla ya uhuru, lilibwa na kuhamisha Z'bar mnataka kusema nini?
Tusijitie uzalendo wakati hatutaki kufuatilia mambo, niliotaja ni baadhi tu ya mengi yaliopo visiwa hivi
"Acha tulipe gharama za ujinga, baada ya kuchezea elimu bure kwa miaka zaidi ya"
Leo nimesikia kumbe nyaraka zenyewe ni zile za umiliki wa baadhi ya visiwa vya Z'bar (Fungu mbaraka)! lkn. kwa hili ni rahisi kufuatilia.
ReplyDeleteNdugu zangu wakati umefika wa kujifunza uzalendo wa Visiwa vyetu (z'bar) pamoja na nchi yetu Tza kwa ujumla!
Ushahidi nilionao unaonesha sisi WAHADIMU ndio wenye kiwango cha chini kabisa cha uzalendo ktk visiwa hivi!
Mfano: wakati mrajisi mkuu alipokua mhindi TOPIWALA kulikua na umakini mkubwa ktk kusajili na kutunza nyaraka zote zilizohusiana na MAMBO MSIIGE lkn. leo hii kuna 'jamaa' yangu pale mambo mchafu koge!
Akija mgeni leo, kesho ana cheti za kuzaliwa! matokeo yake wageni wanakamatwa kwa ugaidi wana passport za Tza tena kutoka Z'bar
Vyeti vya ndoa ndio usiseme! Mashekhe wamepewa vitabu kwa ajili ya vyeti vya ndoa lkn. vikijaa hawendi kufata vyengine kwa vile itabitdi wavilipie, badala yake wanavitoa 'photocopy' athari yake ni kwamba utakuta wanandoa wawili wana vyeti vyenye namba zinazofanana!
Nyaraka na vifaa vingi vinazohusu historia ha Zanzibar zimeanza kupotea tokea siku ya mapinduzj kwa kutetwketezwa na kubomolewa kwa makusudi na hasa baada ya Muungano kwa chuki za kupandikizwa na ujinga wa walioshiriki hayo mapinduzi. Lengo kubwa ni kuiondolea Zanzibar historia ya kweli na kupotezeshea utaifa wake.
ReplyDeleteLeo kama kumepotea nyaraka mbili tatu imekuwa Oman. Serikali ya SMZ inapaswa kumchukulia hatua za nidhami Mwinyi Sadala na wenzake wahariri wa gazeti la serikali Zanzibar Leo pamoja na Mkurugenzi wa Habari wao.