Naibu waziri wa TAMISEMI,Khasim Majaliwa,akipata maelezo na kusaini kitabu cha wageni kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Tasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu chini ya Wizara ya Fedha, Bw, Uli Mtebe
Na Andrew Chale wa Modewji blog
Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu (UTT-PID) inayoshiriki mkutano mkuu wa miaka wa 30 wa jumuia za Serikali za Mitaa Nchini (ALAT), unaofanyika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.Mkutano huo ulioanza Aprili 8 na kutarajiwa kumalizika Aprili 11, UTT-PID imeendelea kutoa elimu na huduma za taasisi hiyo.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa, Mh Hawa Ghasia, akisaini kitabu na kupata maelezo kutoka Afisa Uhusiano Mkuu wa Tasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu (UTT-PID), Uli Mtebe, akiambatana na Afisa Masoko, Bi, Kilave Atenaka .
UTT-PID ambayo imejikita hususani katika upimaji wa viwaja na upangaji wa miji katika maeneo mbalimbali ya Nchi ikiwemo Halimashahuri ya Lindi, Bukoba, Sengerema, Bagamoyo, Chalinze, Morogoro na Halimashahuri nyingine mbalimbali za hapa Nchini.
Aidha, katika maonyesho hayo, banda la UTT-PID limeendelea kutoa elimu na huduma kwa watu mbalimbali kuhusiana na kazi zao zinazofanywa na taasisi hiyo kwa wajumbe wa ALAT na wananchi wanaotembelea banda hilo.
Pia viongozi mbalimbali wa kiserikali akiwemo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia.
Naibu Waziri wanchi Tawala za Mikoa Agrey Mwanri akisaini kitabu cha wageni na kupata maelezo kutoka kwa Afisa Uhusiano Mkuu wa Tasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu (UTT-PID), Uli Mtebe, akiambatana na Afisa Masoko, Bi, Kilave Atenaka
KAZI ZA UTT-PID
Kazi za UTT-PID ni pamoja na Utoaji huduma za ushahuri katika maeneo ya upembuzi yakinifu wa miradi mbalimbali, Uratibu wa fedha na huduma zinazohusiana katika maandalizi ya mapendekezo ya miradi kwa benki au taasisi za fedha, uteuzi wa watoa huduma kuhusiana na maandalizi ya zabuni na usimamizi wa majengo na mali ambao ni utoaji wa huduma fanisi za usimamizi wa majengo yaliyochini ya uangalizi thabiti wa taasisi.
Moja ya mradi uliofanikisha na UTT-PID wa jengo la kisasa la Ushirika Bulding lililopo, Mtaa wa Lumumba, jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment