Habari za Punde

Wanamichezo wa ZSSF na NSSF wakujumuika katika hafla ya Chakula cha Usiku baada ya michezo.

Msanii Othman Makombora akitowa burudani kwa Wanamichezo wa timu za ZSSF na Nssf wakati wa hafla ya chakula cha usiki kilichoandaliwa na Uongozi wa ZSSF. 
Afisa Habari na Uhusiano Ndg Mussa Yussuf akitowa maelezo kwa wageni wao wakati wa chakula cha usiku waliowaandalii wageni wao baada ya michezo ya Bonaza la Michezo ya Pasaka hafla hiyo imefanyika katika Hoteli ya Tembo Shangani Zanzibar. 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfoko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar Ndg Makame Mwadini , akimkabidhi zawadi ya saa maalum Kaimu Mkurugenzi wa NSSF Bi Chiku Matessa, wakati wa hafla ya chakula cha usiku waliowaandalia wageni wao wa michezio ya Bonaza la Michezo mwaka huu limefanyika Zanzibar. 
Meneja wa Huduma kwa Wateja wa ZSSF Ndg. Khamis Filfil akimkabidhi zawadi maalum kwa Viongozi wa Msafara huo wa Wanamichezo wa NSSF,akipokea Meneja Kiongozi Idara ya Uhusiano Huduma kwa Wateja wa NSSF Bi Eunice Chiumbe, mambo ya Zenj hayo. wakati wa chakula cha usiku kilichoandaliwa kwa wageni hao katika hoteli ya Tembo Shangani Zanzibar. 

Meneja wa Huduma kwa Wateja wa ZSSF Ndg. Khamis Filfil akimkabidhi zawadi maalum kwa Viongozi wa Msafara huo wa Wanamichezo wa NSSF, akipokea zawadi hizo Meneja Kiongozi Idara ya Uhusiano Huduma kwa Wateja wa NSSF Bi Eunice Chiumbe,akifurahia zawadi hiyo wakati akikabidhiwa katika ukumbi wa hoteli ya tembo shangani Zanzibar katika hafla ya chakula cha usiku kilichoandaliwa kwa ajili yao.  
Nahodha wa Timu ya NSSF Ndg.Mfaume,Mzee akifurahia zawadi baada ya kukabidhiwa na Nahodha wa Timu ya ZSSF,wakati wa hafla ya chakula cha usiku katika ukumbi wa Tembo hoteli Zanzibar. 

                 Mambo ya msosi baada ya ushindi wa Bonaza la Pasaka kati ya NSSF na ZSSF.
Wanamichezo wakipata chakula maalum kilichoandaliwa kwa ajili yao katika hoteli ya Tembo Shangani Zanzibar.
Wanamichezo wa Bonaza la Michezo ya Pasaka wa ZSSF na NSSF wakipata chakula cha usiku katika hoteli ya Tembo Shangani Zanzibar.
Wachezaji wa timu ya NSSF wakiwa katika ukumbi wa sherehe wakiwa na Kombe lao wa Ushindi wa Bonaza la Michezo ya Pasaka baada ya kuwafunga ZSSF kwa peneti 4--3,mchezo uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.