THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muugano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewateua Majaji wawili wa Mahakama
Kuu ya Tanzania kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani kuanzia Jumamosi iliyopita,
Aprili 24, 2015, taarifa iliyotolewa Dar es Salaam, leo, Alhamisi, Aprili 30,
2025 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) imesema.
Taarifa hiyo imewataja wajaji
hao kuwa ni Jaji Augustine Gherabast
Mwarija na Jaji Stella Ester Augustine Mugasha, ambao wote wamekuwa Majaji wa
Mahakama Kuu ya Tanzania tokea walipoteuliwa Novemba 28, 2006.
Kabla ya uteuzi wake, Jaji
Mwarija alikuwa Jaji Mfawadhi, Kitengo cha Biashara, Mahakama Kuu, Dar Es
Salaam. Kabla ya kuwa Jaji wa Mahakama Kuu alikuwa Msajili wa Mahakama ya
Rufani kati ya mwaka 2003 na 2006.
Aliajiriwa kama Hakimu Mkazi
Daraja la Tatu Februari 2, mwaka 1987, baada ya kupata Shahada ya Sheria mwaka
1986.
Naye Jaji Mugasha, kabla ya
uteuzi wake, alikuwa Jaji Mfawidhi, Dar es Salaam. Alikuwa Mfawidhi, Mahakama
Kuu, Kanda ya Arusha na awali Kanda ya Moshi tangu 2009 hadi alipohamishiwa
Mahakama Kuu, Dar Es Salaam.
Aliajiriwa kama Wakili wa
Serikali mwaka 1983 baada ya kupata Shahada ya Sheria mwaka huo huo, 1983.
Mwisho.
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
30
April, 2015
sawa udumu muungano, lakini hawa wataisaidia nini Zanzibar? ni mahakama ya rufaa ya Tanzania au Zanzibar tuna yetu hii ni kwa Tz bara tu? maana hata juzi niliona Marekani wanacheza mpira timu ya Zanzibar na wengine Tanzania, maana yake Tanzania ndio Tz bara, ile Tanganyika ndo imekuufaaaa.
ReplyDelete