Habari za Punde

Matembezi ya Wapanda Pikipiki Zanzibar Kudumisha Amani na Utulivu katika Kipindi cha Uchaguzi Zanzibar

Wananchi wakiangalia moja ya Pikipiki inayoshiriki Matembezi ya Amani na Utulivu ya Vijana Wapanda Pikipiki Zanzibar yalioandaliwa na Kampuni ya Shirin na Mbunge wa  zamani wa jimbo la Magomeni Mohammed Chombo yalioanzia Magomeni makada na kuelekea Makunduchi na kumalizia katika viwanja vya nje Amani. 
Mshiriki wa Matembezi ya Vijana Wapanda Pikipiki Zanzibar Abdalla Ngwali Makame akiwasili katika viwanja vya Makada Magomeni tayari kwa matembezi hayo.  
Matayarishoya matembezi ya Wapanda Pikipiki Zanzibar katika matembezi ya Amani na Utulivu Zanzibar.
Mkuu wa Polisi Usalama Barabarani akizindua Matembezi ya Amani na Utulivu kwa Vijana wapanda Pikipiki Zanzibar kudumisha hali hiyo katika kipindi hichi cha Uchaguzi, Amewataka Vijana hao kuheshimu sheria za Usalama Barabara wakati wa matembezi yao na kuwaasa kuwa waangalifu wakati wote wa matembezi yao hayo sio resi au kushindana.
Mtayarishaji wa Matembezi hayo Ndg Khalifa Haji Shirin akimsikiliza Mkuu wa Usalama barabarani wakati wa uzinduzi huo
Mratibu wa Matembezi hayo Mbunge wa zamani wa Magomeni Mhe Mohammed Chombo akizungumza na waandishi malengo ya matembezi hayo kuwaweka Vijana pamoja na kudumisha Amani na Utulivu katika visiwa vya Zanzibar katika kipindi hichi cha uchaguzi Mkuu wa Zanzibar.
Mtayarishaji wa Matembezi ya Vijana Wapanda Pikipiki Zanzibar na Mmiliki wa Kampuni ya Shirin Khalifa Haji, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa matembezin hayo ya Vijana Zanzibar wapanda pikipiki. kabla ya kuaza kwa matembezi hayo.
Mpanda pikipiki maarufu Zanzibar katika staili ya kutembea na pikipiki kwa ringi moja Muu Rasta akiwa na mashabiki wake kabla ya kuanza kwa matembezi hayo yalioanzia Magomeni makada kuelekea Makunduchi na kumalizia katika viwanja vya Amani.

          Wananchi wakifuatilia matembezi hayo wakiwa katika barabara ya kwerekwe wakifuatilia matembezi hayo
Askari wa Usalama barabarani akizungumza na wapanda pikipiki kabla ya kuaza kwa matembezi hayo na kuwataka kufuata sheria za usalama barabarani wakiwa katika matembezi hayo.
Wananchi wakifuatilia matembezi hayo wakiwa katika viwanja vya magomeni makada wakisubiri kuaza kwa matembezi hayo.
      Baadhi ya Wananchi wakiwa katika barabara ya mwanakwerekwe wakifuatilia matembezi hayo.



Vijana Wapanda pikipiki wakipita katika maeneo ya barabara ya tunguu Unguja wakielekea Mkoa wa Kusini Unguja na kumalizia katika viwanja vya nje Amani Unguja.






No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.