Na Muhamed Khamis, Univeristy Of Iringa
Sikutaka kuamini kirahisi lakini baada ya kuona mifano kadhaa ilinibidi niamini na kuhisi tulichofundishwa kilikuwa na ukweli ndani yake.
Tukiwa wanafunzi wa Chuo kikuu Iringa, mkufunzi wetu wa somo la Photojournalism alituambia na kutuelekeza kuwa vyombo va habari vya magharibi vinaichafua Africa na kuionesha kwa ubaya ukilinganisha na matokeo mbali mbali ya bara la ulaya.
Nakumbuka mkufunzi huyu (Mr.Aloyce) alitoa mfano tukio la September 11 Nchini Marekani baada ya kubomolewa majengo kadhaa kufuatia mashambulizi ya ndege.
Katika tukio lile hakuna chombo chochote kilichowahi kuonesha picha jinsi watu walivouwawa au kuonekana kwa damu yoyote hile.
Alituambia kila kitu kilifichwa ili watu wasielewe ukweli na huu ndio mfumo wanaoutumia vyombo vya habari ya magharibi kuzilinda nchi zao.
Alitutaka kuvuta kumbukumbu ili tukumbuke tokeo la Westgate Nairobi Kenya au hata lile la Garissa jinsi tv hizi za magharibi zilivoonesha mtapakao wa damu kila sehemu bila hata kuficha kitu kiasi ambacho nathubutu kusema walikwepa kabisa maadili na miiko ya taaluma zao.
Ingawa upo utafauti lakini kwa kiasi kikubwa haitofautiani sana na kwetu,kama hujawahi kufika Zanzibar na umebahatika kusoma magazeti unaweza kudhani ni kesho tu vita vinaweza kutokea Z’bar lakini wapi hali haipo hivyo.
Licha ya Zanzibar kugubikwa na mgongano wa kisiasa lakini vyombo vya habari Tanzania bara hususani magazeti vinaukoleza mgogoro huu kwa maslahi yao binafsi na biashara.
Katika hali isiokuwa ya kawaida sasa magazeti yanayoandika kwa kupotosha ukweli na kuchochea ndio yanayouza kwa kiasi kikubwa.
Vyombo vya habari hivi vinasahau wajibu wao kuwa ni walinzi wa amani badala yake wanageuka kuwa wachochezi wa kutoweka kwa amani.
Nimeshuhudia mara kadhaa maandishi yasiofaa kuandikwa ndio yanayoonekana ukurasa wa mbele kwenye magazeti haya kisa wanataka kuuza huku wakisahau inaweza kuwagharimu wengi maisha yao tukumbuke ya Rwanda.
Nashauri vyombo vya habari visigeuze Zanzibar kuwa soko la bidhaa zao lakini waangalie zaidi thamani ya amani tulionayo ikitoweka nani atawajibika?
Nakumbuka tulifundishwa pia kupoza ukali wa maneno ili kuondosha hasira leo cha kushangaza habari zinaandikwa kama hakuna muhariri jamani.
‘’Niliwahi kuona ukurasa wa mbele(front page) wa gazeti moja kwa sasa limefungiwa likiandika machafuko yaja Z’bar’’ukweli kauli hizi na zinazoshabihiana na uchafuzi wa amani hususani visiwani Zanzibar ifike wakati sasa kutoandikwa yapo mengi ya kuandikwa hakuna ulazima waandishi kuchochea machafuko katika nchi iliotulia na yenye watu wakarimu.
Si kila ukweli usemwao na vyanzo vya habari (source) huhitaji kuandikwa au kusemwa kama ulivo, tujifunze kutumia lugha laini wakati mwengine kupunguza ukali kwa kuhofia machafuko au uhasama zaidi kwa jamii.
Siasa tulizikuta na tutaziacha lakini majeraha ya machafuko ni vigumu kusahaulika kwani malipo yake ni vifo na vilema jambo ambalo daima litabaki kuwa kumbukumbu kwa kila kizazi.
Ifike wakati sasa kila mtu kwa wajibu wake akemee kuchafuliwa Zanzibar na baadhi ya vyombo vya habari tukiamini kuwa walinzi wa amani ya visiwa hivi ni sisi wenyewe hivo tusitoe mwanya kwa kila mmbaya wetu kuichafua kwa mamslah yake .Mungu ibariki Zanzibar mungu wabariki wazanzibar wote.
No comments:
Post a Comment