Habari za Punde

Jumuiya ya Wazazi ya CCM yakabidhi vitendea kazi kwa Uongozi wa Wazazi Mkoa wa Mjini

 Na Mwandishi wetu , Zanzibar.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kitaendelea kuimarisha miundombinu na mazingira rafiki ya kiutendaji kwa kuwapatia vifaa vya kisasa jumuiya mbali mbali za taasisi hiyo ili zifanye kazi kwa ufanisi.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Zanzibar, Najma Murtaza Giga wakati akikabidhi Vifaa mbali mbali kwa Uongozi wa Wazazi Mkoa wa Mjini, huko Afisi ya CCM Amani.

Amesema taasisi hiyo inatakiwa kwenda sambamba na mabadilio ya sayansi na teknolojia kwa kutumia nyenzo za kisasa zitakazowasaidia watendaji wa taasisi hizo kufanya kazi nzuri na kwa haraka.

Aidha amesema chama hicho kitafanya kila kinachowezekana kuhakikisha kinawapatia Vitendea Kazi Watendaji wa CCM kadri ya uwezo wa kifedha unaporuhusu.

Giga amewasihi viongozi mbali mbali wa chama na jumuiya zingine kuunga mkono juhudi zinazofanywa na jumuiya ya wazazi katika kutoa malezi bora ya kitaaluma na kisaikolojia kwa watoto kwa lengo la kutengeneza viongozi makini na weledi wa baadae.

Nae Katibu wa CCM mkoa wa mjini, Mohamed Omar Nyawenga amewataka watendaji wa chama hicho kuwa wabunifu na kutumia weledi kwa kufanya kazi kwa bidi ili kusaiudia chama kutekeleza ilani ya uchaguzi ya 2015/2020 kwa ufanisi ili wananchi waendelee kuiunga mkono CCM katika chaguzi zote zijazo.

Vifaa vilivyotolewa ni Komputa 2, mashine za Printer 2 na mashine za photocopy 4 kwa jumuiya ya wazazi mkoa wa mjini kichama.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.