Habari za Punde

Uzinduzi wa upandaji miti kitaifa Mzambarau Takao, Wete Pemba

 KATIBU Mkuu Wizara ya Kilimo na Maliasi Zanzibar, Afan Othaman Maalim akipanda mti wa mkarafuu katika bonde la Mkanyageni shehia ya Mzambarau Takao Jimbo la Wete, ikiwa ni uzinduzi wa upandaji miti kitaifa iliyofanyika Kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

 NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Mali Asili Zanzibar Dkt Bakari Sadi Ased, akiufukia mche wa mkarafuu baada ya kuipanda, wakati wa zoezi la uzinuzi wa zoezi la upandaji wa miti kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 MMOJA wa Watendaji wa Wizara ya Kilimo Pemba, akibeba miche ya mikarafuu kuipeleka katika sehemu ya kwenda kupandwa wakati wa uzinduzi wa zoezi la upandaji wa mikarafuu kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 BAADHI ya wanawake wakiwa wamebeba miche ya mikarafuu, baada ya kumalizika kwa zoezi la upandaji wa michezo hiyo, huko katika bonde la Mkanyageni Mtambwe.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

 KATIBU Mkuu Wizara ya Kilimo na Mali Asili Zanzibar, Afan Othaman Maalim, akizungumza na wananchi mara baada ya kuzindua zoezi la upandaji wa michezo wa mikarafuu katika bonde la Mkanyageni Mazambarau Takao Mtambwe.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 MKURUGENZI wa Idara ya Misitu Zanzibar Sheha Idrisa Hamdan, akizungumza na wananchi juu ya mikakati ya idara yake kutoa miche ya mikarafuu kwa wananchi bure.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Zanzibar Dkt Bakari Sadi Ased, akizungumza na wananchi wa Mzambarau Takao mara baada ya kumaliza kazi ya upandaji wa miti ya Mikarafuu kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.