Habari za Punde

Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ Yakabidhi Msaada wa Dawa na Vifaa kwa Kambi ya Kipindupindu Zanzibar.

 Baadhi ya Vifaa vilivyotolewa na Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ kwa ajili ya Kami ya Kipundupindu Zanzibar vimekabidhiwa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ndg Juma  Ameir, wa pili kushoto akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa Vifaa na Madawa kwa Wizara ya Afya Zanzibar kwa ajili ya Kambi ya Kipindupindu, kulia Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk Juma Malik.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ndg Juma Ameir akimkabidhi vifaa na Madawa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Dk Juma Malik, hafla hiyo imefanyika katika Makao Makuu ya PBZ Islamic Mpirani Jengo la Bima Zanzibar. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ndg Juma Ameir akimkabidhi vifaa na Madawa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Dk Juma Malik, hafla hiyo imefanyika katika Makao Makuu ya PBZ Islamic Mpirani Jengo la Bima Zanzibar. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Juma Ameir akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa madawa kwa Wizara ya Afya Zanzibar. 







Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dk Juma Malik akizungumza na kutowa shukrani kwa Uongozi wa PBZ kwa msaada wao huo wa madawa kusaidia Kambi ya Kipundupindu Zanzibar. 

Mkurugenzi Kinga Wizara ya Afya Zanzibar Dk Mohammed Dahoma akijibu swali la waandishi wa habari waliotaka kujuwa hali ya wagonjwa katika kambi za kipindupindu, na kueleza kwa sasa kasi ya ugonjwa huo imepungua kwa kiasi na kesi nyingi wanazozipata kambi hapo ni kupelekwa watoto wadogo kuwa na maradhi hayo.
Maofisa wa Benki ya Watu wa Zanzibar wakifuatilia hafla ya kukabidhi Vifaa na Madawa kwa Kambi ya Kipindupindu Zanzibar vilivyotolewa na Benki hiyo hafla hiyo imefanyika Makao Makuu wa PBZ Islamic Mpirani Zanzibar.
Wafanyakazi wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) wakimsikiliza Dk Mohammed Dahoma akitowa maelezi ya maradhi ya kipindupindu kwa waandishi wa habari wakati wa hafla ya kukabidhiwa misaada ya madawa na vifaa kwa ajili ya kambi hiyo vilivyotolewa na (PBZ) na kusema kasi ya ungonjwa huo kwa sasa imepundua na kesi wanazozipata katika kambi hiyo ni kuletwa watoto wadogo. 




No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.