Habari za Punde

Chuo cha ZIBRET Chatowa Mafunzo ya Maalum kwa Ajili ya Kujiandaa na Kustaafu Wafanyakazi Zanzibar.

Mratibu wa Mafunzo Ndg Fahim Hassan,kwa Wafanyakazi wanaojiandaa kustaafu Kazi Zanzibar ili kuwajengea Uwezo wa kubuni miradi na Kujiandaa kustaafu. mafunzo hayo yalikuwa kwa siku nne na kuwashirikisha Wazee 10 kwa awamu ya mwazo wa mafunzo hayo yaliofanyika katika Chuoni hicho Jengo la ZIBRET Mwanakwerekwe Zanzibar.  
Mkuu wa Chuo cha Zanzibar Institute of Business Research and Technology Ndg Ali Suleiman akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Veti kwa Wahitimu ya Mafunzo ya Maalum kwa Ajili ya Kujiandaa na Kustaafu yaliowashirikisha Wastaafu 10, waliopata mafunzo hayo ya kuwajengea Uwezo wa kubuni Miradi wakati wakiwa nje baada ya kustaafu.
Wafanyakazi Wastaafu wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa Vyeti baada ya Mafunzo yao 
Mkurugenzi wa Chuo cha ZIBRET Ndg Khatib Mjaka Hamad akitowa nasaha zake kwa Wahitimu wa Mafunzo ya Kujiandaa na Kustaafu yaliotolewa na Chuo chao kwa Wafanyakazi hao Wastaafu ili kuwajengea Uwezo wa kujitengemea kwa kuibuwa miradi ya maendeleo yao wakiwa nje baada ya kustaafu.
Mshauri wa Chuo cha ZIBRET Salum Ali, akizungumza na kutowa nasaha zake kwa wahitimu hao baada ya kupata mafunzo ya kujijengea uwezo wanapostaafu kazi ili kuweza kuibua miradi ya kuwaendeleza maisha yao ya kila siku mafunzo.Hafla hiyo imefanyika katika Chuo hicho jengo la ZIBRET Mwanakwerekwe Zanzibar. No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.