Habari za Punde

Kongamano la Wakulima wa Mbogamboga Lililoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la VSO



Afisa Mratibu wa Mradi wa ICS Casha Project Franklin Kebelo akizungumza wakati wa Kongamano hilo la Wakulima wa Kilimo cha Mbogamboga Zanzibar lililofanyika katika ukumbi wa SUZA Majestik Zanzibar na kuwashirikisha Wakulima wa sehemu mbalimbali za Unguja.  
Wakulima wa Mbogamboga wakimsikiliza Mratibu wa Mradi wa Cash Project Zanzibar.
Vijana wa kujitolewa wa Shirika la VSO wakiwa katika kongamano hilo lililoandaliwa na VSO na ICS lililofanyika katika ukumbi wa SUZA Zanzibar.
Kijana wa Shirika la VSO Joseph Silverman akitowa mada wakati wa Kongamano hilo la Wakulima wa Mbogamboga Zanzibar lililofanyika katika ukumbi wa SUZA Zanzibar. 
Wakulima wa mbogamboga wakifuatilia mafunzo wakati wa Kongamano hilo la Wakulima wa Mbogamboga Zanzibar lililoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la VSO.
Bwana Shamba NdgHaji Ali Mtumwa akitowa maelezo jinsi ya kutayarisha shamba hai kwa wakulima wa mbogamboga Zanzibar wakati wa Kongamano la Wakulima Zanzibar lililofanyika katika ukumbi wa SUZA Majestik Zanzibar.
Mtaalamu wa Kilimo cha mbogamboga Suleiman Nassor akitowa maelezo ya utaalamu wa kilimo hicho wakati wa Kongamano hilo la Wakulima wa Mbogambago Zanzibar, Mradi huo wa kilimo cha mbogambogo uko chini ya mradi wa VSO. 

Mfanyabiashara za makotelini akitowa maelezo jinsi ya bidhaa za mbogambago za kilimo hai bidhaa hizo hupendwa sana katika mahoteli ya Zanzibar na wageni wanaofika katika mahoteli hayo kwa kuwa na harufu hali ya matunda hayo na bei yake iko juu kuliko ya kilimo cha kisasa kutumia mbolea za kemikali.
Mtaalamu wa Mbegu Bi Fatma Mwinyiwesa akitowa maelezo ya Mbegu bora kwa Wakulima wakati wa Kongamano hilo lililo chini ya mradi wa Shirika lisilo la Kiserikali la VSO. linalotowa elimu ya kilimo cha mbogamboga kwa wakulima wa Zanzibar.




Wakulima wakichangia kuhusiana na kilimo hai wakati wa Kongamano hilo.
Vijana wa VSO wakiwa katika ukumbi wa Kongamano katika Chuo cha SUZA Majestiki Zanzibar.
Mkulima wa mbogamboga akionesha moja ya midhaa za kilimo hicho boga wakati wa maonesho ya bidhaa zao wanazolima kwa kilimo hai bila ya kutumia mbolea za kemikali na kutumia mbolea za kienyeji za mavi ya kuku na kadhalika.

Wakulima wa mbogamboga wakiwa katika maonesho na kuuza bidhaa zao kwa wananchi waliohudhuria kongamano hilo.
Wakulima wa kilimo cha mbogamboga wakionesha bidhaa zao wakati wa Kongamano hilo lililoandaliwa na VSO katika ukumbi wa SUZA majestiki Zanzibar. 
Vijana wa Kujitolewa wa Shirika la VSO wakiwa katika picha ya pamoja na wakulima wa Mbogamboga Unguja baada la Kongamano la Wakulima hao lililoandaliwa na VSO katika ukumbu wa SUZA majestiki Zanzibar.

1 comment:

  1. This is a good event, I really appreciate the effort you have shown to the public. Keep it up.

    Donald - UWZ

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.