Habari za Punde

Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya Azungumza na Waandishi wa Habari Kuhusu Maradhi ya Kipindupindu.

Mkurugenzi Kinga Wizara ya Afya Zanzibar Dk Mohammed Dahoma akizungumza na waandashi wa habari na kutoa taarifa za kila wiki kuhusiana na maendelea ya maradhi ya kipindupindu Zanzibar, kwa kufikia wiki hii wagonjwa wa kipindupindu wamepungua katika Kambi hizo na kufikia wagonjwa 45 hadi anatoo taarifa hiyo kwa waandishi wa Habari Zanzibar wa vyombo mbalimbali, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi Mmoja Zanzibar na kuwataka Wananchi kujenga tabia ya kuchemsha maji ya kunywa. Na kuweka mazingira safi katika makaazi yao kuepusha maradhi ya matumbo.  
Mkurugenzi Kinga Wizara ya Afya Zanzibar Dk Mohammed Dahoma akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kutowa taarifa ya maradhi ya kipindupinduzi Zanzibar. na kueleza kwa sasa wanafanya zoezi la kuaza kufungua baadhi ya mikahawa katika zoni A maeneo ya Mji Mkongwe kwa kuwafanyia uchunguzi wafanyakazi wa migahawa hiyo na maeneo ya biashara hizo zoezi hilo linaendelea na likiwa tayari watatoa taarifa kwa wananchi. 


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.