Habari za Punde

Tanzania na Fiji za Aanzisha Uhusiano wa Kidiplomasia

Na. Mwandishi Maalum, New York

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Fiji zimekubalia na kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia katika ngazi ya Mabalozi .

Mwakilishi wa Kudumu wa  Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, na Mwakilishi wa Kudumu wa Fiji katika Umoja wa Mataifa Balozi  Peter Thomson ndio waliotia saini hati za kuanzishwa kwa uhusiano huo kwa niaba ya serikali zao katika hafla fupi iliyofanyika siku ya Alhamisi katika Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania.

Fiji inakuwa nchi ya tatu baada ya  Malta na Equador ambazo tayari zimekwisha anzisha uhusiano wa kidiplomasia na Tanzania katika ngazi ya Mabalozi.Kama ilivyokuwa kwa nchi hizo mbili hati za makubaliano hayo zitawasilishwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Wakizungumza mara baada ya kubadilishana hati, wawakilishi hao pamoja na kuonyesha kufurahishwa na uhusiano huo, pia walielezea namna gani wanavyoweza kukuza ushirikiano katika masuala mbali mbali yenye maslahi kwa pande hizo mbili hapa Umoja wa Mataifa na nje ya Umoja wa Mataifa.“Ni kwa muda mrefu serikali yangu (Fiji) imekuwa ikitamani sana kuwa na uhusiano na Tanzania,  labda pengine niongeze kwamba sisi wananchi wa Fiji baadhi ya vizazi vyetu asili yake ni Tanganyika (Tanzania) kwa hiyo uhusiano huu utaimarisha zaidi siyo tu kutambua na kuthamini kule tulikotoka, lakini pia  tunayo  mambo ambayo tunaweza kubadilishana uzoefu kwa manufaa ya nchi zetu na watu wake”. Akasema Balozi.

Kwa upande wake, Balozi Tuvako Manongi amemwambia Balozi Thomson kwamba,  nchi hizo mbili zimefungua ukurasa mpya. Na akaongeza . “ nimewahi kutembelea Fiji,ingawa ilikuwa ni kwa muda mfupi lakini niliweza kujionea na kujifunza kilimo cha kisasa na endelevu na pia zao la nazi ambalo hata kwetu ( Tanzania) ni moja ya zao muhimu sana, kwani ninaamini kwamba kwa kuanzisha uhusiano huu tunayo mengi ya kujifunza kutoka kwetu.Jamhuri ya Fiji ni Kisiwa kilichoko katika Bahari ya  Pacific ya Kusini ( South Pacific Ocean) na lilikuwa koloni la  Uingereza kabla ya kujipatia uhuru wake mwaka 1970.

Uchumi wa nchi hiyo pamoja na mambo mengine, unaendeshwa kwa kiasi kikubwa na sekta za utalii,  madini, bidhaa za misitu,  uzalishaji wa sukari,   mazao yatokanayo na nazi,  pamoja na viwanda vidogo vya pambana  pia  Fiji inatengeneza nguo…..

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.