Habari za Punde

Jumuiya ya Sadakatasi ya Uturuki kwa kushirikiana na Jumuiya ya Muzdalifah yatoa misaada kisiwa cha Tumbatu Jongoe

 Wawakilishi wa Jumuiya ya Sadakatasi ya Uturuki wakiwa na wenyeji wao wa Jumuiya ya Muzdalifa ya Zanzibar wakiwasili katika kisiwa cha Tumbatu Jongowe kwa ajili ya kutoa misaada mbalimbali yenye thamani ya shiling milioni kumi na nane.
  Wananchi wa Tumbatu Jongoe wakishusha vipolo vyenye misaada mbalimbali kwaajili ya mwezi Mtukufu wa Ramadhan.  

 Baadhi ya wazee wa Kisiwa cha Tumbatu Jongoe wakiwa kwenye foleni kwaajili ya kupokea misada mbalimbali iliyotolewa na Jumuiya ya Sadakatasi ya Uturuki.
 Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Sadakatasi ya Uturuki Emrah Eugin akimkabidhi kipolo chenye Mchele, unga, sukari na mafuta ya kula kwa ajili ya mwezi Mtukufu wa Ramazan mmoja wa wazee wa Tumbatu Jongoe.
 Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Sadakatasi ya Uturuki Emrah Eugin wakatikati na mwenziwe Huseyin Kursun (kushoto) wakiwapa nguo watoto wa Tumbatu Jongoe ikiwa ni miongoni mwatarati iliyojiwekea Jumuiya hiyo.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Sadakatasi ya Uturuki Emrah Eugin akiagana na watoto wa kisiwa cha Tumbatu Jongoe, mara baada ya kumaliza kutoa sadaka ya vitu mbalimbali vyenye thamani ya milioni kumi na nane. Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.