Habari za Punde

Tukiwaamini na Kuwawezesha Vijana Itakuwa Rahisi Kutekeleza Agenda 2030- JK

Rais Mstaafu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete jana  jumanne alitoa mhadhara wa  13 wa Kumbukumbu ya  Rafael M. Salas ulioandaliwa  Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu ( UNFPA), mhadhara huo ulikuwa ni sehemu ya vikao vya mwaka vya  Bodi na Mifuko ya Umoja wa Mataifa vinavyoendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Pamoja naye Meza Kuu ni  Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA Dr. Babatunde Osotimehin, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Jan Elliason, Rais wa Bodi, na Balozi Carmelita R. Salas, mjane wa Bw.  Rafael M. Salas
Sehemu ya  washiriki wa mhadhara wa 13 kumbukumbu ya Rafael M. Salas, uliofanyika siku ya Jumanne ambapo  mzungumzaji  mkuu alikuwa ni Rais Mstaafu  Mhe. Jakaya Kikwete. Tanzania ni  Mjumbe wa  UNFPA.
Mhe Jakaya Kikwete akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa muda  mfupi kabla ya kuanza kwa mhadhara wa 13 wa kumbukumbu ya Rafael  Salas uliofanyika katika ukumbi wa ECOSOC katika Umoja wa Mataifa.
Dr. Babatunde  Osotimehin akielezea jambo kwa Mhe Rais  mstaafu Jakaya Kikwete,  wengine ni Balozi Carmelita Salas, Mjane wa Rafael M. Salas aliyekuwa Mkurugenzi  Mtendaji wa  kwanza wa UNFPA.

Na MwandishiMaalum, New York
Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amesema,     ingawa idadi kubwa ya vijana wasiokuwa na uhakika wa maisha yao wala kazi zenye tija na staha wapo katika nchi zinazoendelea, dunia katika ujumla wake inapashwa kuonyesha utashi wa kisiasa na udhubutu wa kuwekeza kupitia vijana.

Amesema,  mazingira ya mamilioni ya vijana kukaa

bila shughuli ya aina yoyote kunatoa mwanya kwa 

vijana hao kurubuniwa na kutumiwa na watu wasio 

kuwa na nia njema na hivyo kutishia hali ya Amani,  

usalama na ustawi wa mwanadamu na hatimaye 

kushindwa kufikia au kupata faida za kidemograsia 

na maendeleo endelevu.

Mhe. Kikwete ameyasema hayo jana(jumanne) hapa 

Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, wakati alipotoa 

mhadhara wa  13 wa kumbukumbu ya Rafael M. 

Salas. Mhadhara huu ambao mada yake ilikuwa ni “ 

kuwekeza kwa vijana ili kupata faida ya kidemokrasia 

na maendeleo endelevu” uliandaliwa na Shirika  la    

Umoja wa Mataifa kuhusu Idadi ya Watu( UNFPA) 

ikiwa ni sehemu ya mikutano ya mwaka ya Bodi za 

Mashirika na Mifuko iliyopo chini ya Umoja wa 

Mataifa.

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria na kushiriki 

mhadhara ni pamoja  na Naibu Katibu Mkuu wa 

Umoja wa Mataifa,  Bw. Jan Eliasson, na Mkurugenzi 

Mtendaji wa UNFPA  Dr. Babatunde Osotimehin ,  Bi. 

Carmelita R. Salas ambaye ni Mjane wa Bw.  Rafael 

Salas aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa  kwanza wa  

UNFPA, Mabalozi na wataalamu mbalimbali.

“Tafiti na taarifa mbalimbali zikiwamo za Umoja wa 

Mataifa, zinaonyesha wazi ongezeko la  idadi kubwa 

yavijana wanaokadiriwa kufikia 1.8 bilioni idadi ambayo ni hazina na raslimali kubwa, lakini pamoja na uwingi wao, wengi bado wanaishi katika hali ya umaskini uliokidhiri,  na ukosefu wa fursa mbalimbali ambazo zingewezesha kuishi maisha yenye staha”.
akasema Kikwete

Na kuongeza kuwa, kati ya vijana hao 1.8 bilioni, 74 

milioni hawana ajira akiwaelezea kama vijana 

wanaosubiri treni kando ya reli, treni ambayo 

haiji.Mazingira haya yanadhihirisha upotevu wa raslimali kubwa ambayo imewekezwa kwa vijana hao na ambao wamepoteza matumaini.

Akafafanua zaidi kwa kutoa takwimu mbalimbali zinazoonyesha tofauti ya faida za kidemokrasia kati ya mabara ya Ulaya, Asia, Amerika ya Latini na Afrika ikiwa ni pamoja na utofauti wa matumizi ya raslimali watu kwa nchi zile ambazo zimethubutu kuwekeza kwa vijana.

Rais Mstaafu Kikwete katika mhadhara wake huo na 

ambao ulipokelewa vema sana na wajumbe 

waliohudhuria, pia ametoa vielelezo vya kitakwimu 

vinavyoainisha namna gani  bara la  Afrika lilivyo 

nyuma karibu katika ikielemewa kila eneo kuanzia 

upatikanaji na utoaji wa huduma za uzazi salama,  

idadi ya wakunga wenye elimu ya kutosha, 

upatikanaji wa huduma za afya,  elimu,  maendeleo ya kijamii na yenye tija na stahiki na kiwango  cha matumizi ya njia za kisasa za uzazi wa mpango.

“Vijana wakiwezeshwa, wakiaminiwa,  wakipewa fursa 

na wakithibitishwa wanauwezo mkubwa sana wa 

kuleta mabadiliko. Tunatakiwa kuwaamini, 

tunatakiwa kuwashirikisha na kuzisikia sauti zao” amesema.

Na kuongeza kuwa , mipango na sera zinazoandaliwa 

kwa ajili yao vijana ni vema zikawashirikisha na 

kuzingatia mawazo, maoni na matakwa ya vijana.
“ 
Haya na mengine mengi kwa kutekelezwa kwa 

kuzingatia mazingira ya kila nchi na vipaumbele 

vyake,  tunaweza kugema nguvu kazi hii kubwa 

kujiletea maendeleo endelevu pasipo kumwacha 

yeyote nyuma” akasisitiza Rais Mstaafu.

Katika hotuba yake hiyo iliyosheheni takwimu na 

utafiti wa kisayasi, siyo tu kwamba imeainisha hali 

halisi ya mazingira waliyomo vijana bali pia 

imechochea majadiliano ya kina.

Baadhi ya mambo  ambayo ameyatilia mkazo ni 

pamoja na umuhimu wa jamiii kuzingatia usalama na 

wa mpango na kuwanadi idadi ndogo ya watoto na 

ambayo wazazi wataweza kuimu du na elimu 

itakayokidhi mahitaji ya soko la ajira lishe bora na 

uchumi imara na endelevu.

Akimkaribisha Rais Mstaafu kuzungumza,  Naibu 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Elliason 

pamoja na  mambo mengine alimwelezea Mhe. 

Kikwete kuwa ni kiongozi mpenda amani na aliyemstari wa mbele katika kusimamia afya ya mama namtoto.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.